BANDA MEDIA BLOG

BALOZI MNDEME AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA MFALME CARL XVI GUSTAF WA SWEDEN

 

                                                                 ....................

Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mheshimiwa Swahiba H. Mndeme, amewasilisha rasmi Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden katika hafla maalum iliyofanyika tarehe 22 Mei 2026, kwenye Kasri la Mfalme wa Sweden lililopo jijini Stockholm.

Hafla hiyo ya kidiplomasia ni ishara ya kutambuliwa rasmi kwa Balozi Swahiba kama Mwakilishi rasmi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Sweden.

Aidha, hatua hiyo inafungua ukurasa mpya wa kuendelea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu, wa kirafiki na kidiplomasia kati ya Tanzania na Sweden. 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG