BANDA MEDIA BLOG

YANGA YAIONDOA SIMBA SC KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA OKELO AKISHAINI

 

Mchezaji Alan Okello Tangu alipojiunga na Timu ya Yanga katikati ya msimu huu akitokea kwao nchini Uganda mpaka sasa amehusika na Magaoli 18 na kuwafanya Mabingwa hao  watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo, Mei 25, 2026, kwenye uwanja KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam.

Hii ni miujiza ya Allan Okello… Star Boy tayari amefunga magoli 11 huku akitoa assists 7 ndani ya muda mfupi tangu atue kwenye Ligi.

Mabao ya Yanga SC yalifungwa na Duke Abuya pamoja na Allan Okello aliyefunga mabao mawili, huku bao la Namungo FC likifungwa na Hassan Kabunda. yameirejesha yanga kileleni mwa msimamo wa ligi

Kufuatia matokeo hayo, Yanga SC imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 60, huku watani wao Simba SC wakishuka hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 58.

Timu zote zimecheza michezo 25, zikibakiwa na michezo mitano kabla ya kumalizika kwa msimu wa ligi unaoendelea kuwa na ushindani mkubwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG