BANDA MEDIA BLOG

DIDIER DROGBA ALIVYOTIKISA BUNGE LA TANZANIA

 

Didier Drogba Atikisa Bunge la Tanzania
Didier Drogba Atikisa Bunge la Tanzania

Shangwe​ zilitawala katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma  Mei 4, 2026, baada ya gwiji wa soka duniani na nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ivory Coast na mchezaji wa Chelsea, Didier Drogba kutambulishwa mbele ya wabunge na wageni waalikwa.

​Drogba, ambaye aliwasili nchini jana kwa mwaliko rasmi wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amepata mapokezi ya kipekee na kuwa kivutio bungeni.

​Lengo la ziara ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 48, ambaye miongoni mwa wachezaji bora walioweka alama katika soka barani Afrika na duniani, ni kuunga mkono jitihada za kukuza michezo na utalii nchini.

Drogba anakumbukwa kama mshambuliaji mwenye nguvu na ushawishi mkubwa, hasa katika klabu ya Chelsea ambako alicheza kwa mafanikio makubwa.

​Klabu nyingine alizowahi kuchezea nyota huyo ni ​​Olympique Marseille (Ufaransa), ​Shanghai Shenhua (China), ​Galatasaray (Uturuki), ​Montreal Impact (Canada/MLS) na ​Phoenix Rising (Marekani)

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG