AFISA michezo wa Jiji la Dodoma, Neema Kilongola amewahamasisha wakazi wa Jiji la Dodoma kujitokeza kwa wingi katika mashindano ya Mwenge Super Cup yanayotarajia kuanza mnamo tarehe 15/05/2026 na kutamatika tarehe 16/05/2026 ikiwa ni mara ya kwanza kwa mashindano haya kufanyika ndani ya Jiji
la Dodoma.
Aliyasema hayo katika mahojiano aliyoyafanya katika Kituo cha Redio Dodoma FM, ndani ya kipindi cha michezo cha Bab Kubwa.
Mashindano hayo yatahusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa kikapu,
volleyball na netball itakayo jumuisha watu wa rika zote, yatakayofanyika katika viwanja tofauti tofauti ambapo kwa mpira wa miguu utafanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma huku Volleyball,Netball na Mpira wa Kikapu vitafanyika Chinangali Park.

