BANDA MEDIA BLOG

WAZAZI NA WALEZI WAMEKUMBUSHWA KUTIMIZA WAJIBU,KUJENGA FAMILIA YA KRISTO


Na Maiko Luoga   - Dodoma

Wazazi na walezi wameshauriwa kulea watoto katika misingi bora ya Imani ya Kristo ili kuandaa familia zenye maadili mema za kumpendeza Mungu pamoja na kutoa mchango Chanya katika Kanisa, Jamii na Taifa.   

Wito huo umetolewa na Kasisi Can. Dkt. Samwel Maduma, Mkuu wa Chuo cha Thiolojia Morogoro, (Morogoro Bible College) alipohubiri kwenye Ibada ya Misa Takatifu Jumapili 17 mei 2026, Siku ya Bwana  baada ya kupaa.

Ibada hiyo ilifanyika katika Kanisa la Watakatifu Wote Chadulu, Dayosisi ya Central Tanganyika DCT, Kanisa Anglikana Tanzania ilibeba Wazo Kuu, Ahadi ya Roho Mtakatifu, Dkt. Maduma alikumbusha wazazi na walezi kushika vyema wajibu wao ili kuandaa familia bora zenye kuishi Imani ya Kristo.

“Biblia Takatifu kupitia Yoshua 24:13 – 16 inatukumbusha kuchagua Mungu Tutakae mtumikia, maandiko haya yanatukumbusha kumsikiliza Roho Mtakatifu ili aweze kutuongoza vyema” alisema Kasisi Can. Dkt. Samwel Maduma.

Aidha ilifanyika Ibada ya Sakramenti ya Ubatizo Mtakatifu kwa mtoto mmoja ambae aliingizwa rasmi katika Kundi la Kristo.

Misa hiyo iliongozwa na Kasisi Mwenyeji, Emmanuel Nyombe ambae aliwatangazia waumini kuwa, Jumapili ya Pentekoste 24 mei 2026 itafanyika Ibada ya ufunguzi wa Semina ya Neno la Mungu kisha kuendelea hadi 31 mei 2026, Mwimbaji Ambwene Mwasongwe atafundisha na kuhudumu kwa njia ya uimbaji.








Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG