BANDA MEDIA BLOG

WAVUTAJI NA WASAMBAZAJI WA BANGI IYUMBU WATAFUTIWA DAWA

 

                                               Mkaguzi wa Polisi Daud Matala
                                                    .........................

                           John Israel,  Banda Media Dodoma Tanzania

DIWANI wa kata ya Iyumbu, jijini Dodoma Sadik Mponyamili amesema kata imejizatiti kuchukua hatua kazi dhidi ya yoyote atakayebainika kujihusisha na vya vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu ikiwa ni pamoja na utumiaji na usambazaji wa Dawa za Kulevya ikiwemo Bangi.

 

akiongea hivi karibuni na channel ya mtandaoni ya Banda Media katika uwanja wa shule ya msingi iyumbu kulikokuwa na mashindano ya Mwenge Cup, Mponyamili amesema kimsingi hali si shwali kwani Ofisi yake imekuwa ikipokea taarifa ya matumizi na usambazaji wa Dawa za Kulevya ikiwemo Bangi pamoja na matukio ya udokozi na uporaji yanayofanywa na vibaka kuwavamia kimama wanaoenda kuuza bidhaa za mbogamboga na matunda nyakati za alfajiri...

"kutokana na hayo tumeanzisha doria kwa kushirikisha wananchi, lakini pia jeshi letu la polisi ambapo hatua za upelelezi zinaendelea ambapo atakayebainika kujihusisha na uhalifu wowote atachukuliwa hatua kali lengo likiwa ni kuomesha matukio hayo", amesema

Kwa upande wake Polisi Kata wa kata ya Iyumbu Mkaguzi wa Polisi Daud Matala amesema miongoni mwa taarifa ambazo wamezipata kutoka kwa wananchi wema ni pamoja na Wizi ukiwemo wa pikipiki, kufuangua baadhi ya spea za pikipiki, Udokozi na matukio mengine madogomadogo.

amesema kazi ya jeshi la polisi ni kubaini, kuzuia na kutanzua Uahalifu. "tayari tumeanzisha mkakati wa kuongea na wananchi tukianza na kutoa elimu ili kujua uhalifu ni nini, upo wapi na jinsi ya kuutolea taarifa katika kituo chetu cha polisi kilichopo Chimwaga UDOM",amesema

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG