BANDA MEDIA BLOG

WATANZANIA Waishio Nchini Afrika Kusini Kurudishwa Tanzania Kesho

WATANZANIA Waishio Nchini Afrika Kusini Kurudishwa Tanzania Kesho

WATANZANIA Waishio Nchini Afrika Kusini Kurudishwa Tanzania Kesho

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, John Bwana amesema Watanzania waliopo Nchini humo wamekusanyika na wapo tayari kurejea Tanzani.

Akizungumza leo katika Ukumbi wa City View Jijini Durban, Balozi Bwana amesema Kundi kubwa la Watanzania limejitokeza kuitikia wito wa kampeni ya “Anarudi Nyumbani kwa Mama”, ambayo imekuwa ikiendeshwa kwa muda na sasa imezinduliwa rasmi Jijini Durban.

Amesema Watanzania hao walijiandikisha kwa hiari kwa ajili ya kurejea Tanzania kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Hadi sasa zoezi linaendelea hapa ndani na Watanzania wengi wamejitokeza, Wanawake, Wanaume, Watu wenye umri mdogo, wa kati na watu wenye umri mkubwa. Wote wamejitokeza kwa furaha kubwa na kwa utayari, kwa dhamira yao wenyewe kuondoka na kurejea nyumbani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Balozi Bwana.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG