Katibu Mkuu wa Ushirika wa Kanisa Anglikana Ulimwenguni (Anglican Communion) Askofu Anthony Poggo, akizungumza jambo wakati alipokuwa akitoa salamu Katika Utulivu wa Maaskofu na wake zao unaoendelea katika Dayosisi ya Biharamulo mkoni Kagera.
.......................
Na Rev. Rev. Maiko Luoga - Biharamulo.
Katibu Mkuu wa Ushirika wa Kanisa Anglikana Ulimwenguni (Anglican Communion) Askofu Anthony Poggo amewasili nchini Tanzania kwa lengo la kuona hatua za maendeleo ya Kanisa.
Mara baada ya kuwasili nchini Tanzania 27 Agosti 2026, Katibu huyo Raia Toka Nchini Sudani ya Kusini amekwenda moja kwa Moja kwenye Utulivu wa Maaskofu na wake zao unaofanyika Katika Dayosisi ya Biharamulo Mkoani Kagera
Askofu Poggo amepata nafasi ya kutoa Salaam kwa Maaskofu wa Kanisa Anglikana Tanzania na wake zao wanaoendelea na Utulivu katika Ukumbi wa Hoteli ya Ebeneza, (Ebenezer Conference Hall) Dayosisi ya Biharamulo.
Utulivu Huo uanendelea ambapo Ibada ya Awali iliyofanyika Agosti 27, 2026 imeongozwa na Askofu Given Gaula wa Dayosisi ya Kondoa aliyetoa Tafakari ya Neno la Mungu, akisaidiwa na Askofu Jackson Sosteness wa Dayosisi ya Dar es Salaam na Kasisi Can. Charles Lundu Askofu Mteule Dayosisi ya Handeni.
"tweka mpaka kilindini", ndilo Neno Kuu linalotumika katika Utulivu huo likitoka katika Injili ya Luka Mtakatifu 5:4-11, Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
Ratiba ya Utulivu wa Maaskofu na Wake zao, Imeandaliwa na Ofisi Kuu ya Kanisa Anglikana Tanzania kupitia Askofu Mkuu Maimbo Mndolwa, unatarajiwa kuhitimishwa siku ya Jumamosi Tarehe 29 Agosti 2026
The Anglican Church of Tanzania (ACT)
Dwt Habari
Anglican Communion







