BANDA MEDIA BLOG

CHARITY NGILU AMTUHUMU RAIS KENYATTA KWA UPENDELEO KATIKA VITA DHIDI YA RUSHWA


Waziri wa Ardhi wa Kenya aliyesimamishwa kazi, Bi. Charity Ngilu, amemtuhumu rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyingine kwa kuonyesha upendeleo katika mapambano dhidi ya rushwa.

Bi. Ngilu amesema kitendo cha rais kushindwa kumsimamisha kazi Waziri wa Wizara ya Ugatuaji Madaraka Bi. Anne Waiguru kufuatia tuhuma nzito za rushwa katika wizara yake, kumeifanya nchi kuwa kituko.

Amesema kuwa heshima ya taifa la Kenya ipo mashakani na Wakenya wameanza kupoteza imani na serikali yao katika mapambano dhidi ya rushwa, kutokana na kuwepo upendeleo na kukosekana utashi wa kisiasa.
Waziri wa Wizara ya Ugatuaji Madaraka Bi. Anne Waiguru

Waziri wa Ardhi aliyesimamishwa Bi. Charity Ngilu

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG