BANDA MEDIA BLOG

MGOMBEA URAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP AZOMEWA NA KUITWA MBAGUZI



Mgombea urais wa Marekani Donald Trump amekumbwa na dhahama ya kuzomewa kwa sauti iliyokuwa kimuita mbaguzi wakati ufunguzi wa shoo ya uchekeshaji jana usiku.

Kitendo hicho kimefanywa na mchekeshaji Larry David, ambaye alisema ni mzaha katika kupaza sauti ya kundi la kudai haki za Walatino, waliokerwa na kauli za Bw. Trump kuhusiana na Wahamiaji wenye asili ya Mexico.


Waandamanaji wenye asili ya Kilatino walikuwa nje ya studio za NBC Jijini New York wakati shoo hiyo ikiendelea.

Wakati akitangaza nia ya kuwania urais kwa tiketi ya chama cha Republican Bw. Trump aliwaelezea wahamiaji wa Mexico kama wabakaji na wauza dawa za kulevya.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG