Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akitoa ufafanuzi kwa
wanabari (hawapo pichani) kuhusu uandishi bora wa habari za Mahakama
wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za
Mahakama leo jijini Dar es salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (kushoto) na Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Allan Lawa (kulia) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za Mahakama yaliyoandaliwa na Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam
Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari namna wanavyoweza kuandika habari za Mahakama kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao.
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande leo jijini Dar es salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (kushoto) na Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Allan Lawa (kulia) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za Mahakama yaliyoandaliwa na Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam
Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari namna wanavyoweza kuandika habari za Mahakama kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao.
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia
mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo ya
kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama leo jijini Dar es
salaam.
Picha/Aron Msigwa –MAELEZO.
………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Dar es salaam.
Waandishi wa
habari nchini wametakiwa kuzingatia weledi wa taaluma zao wanapoandika
habari za Mahakama ili kuepuka kuandika habari zinazowatia hatiani
watuhumiwa na kushindwa kutofautisha kati ya mshitakiwa na mtuhumiwa
pamoja na haki zake.
Akifungua
mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama leo jijini
Dar es Salaam, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande amesema
waandishi wa habari wanalojukumu la kuwapatia wananchi taarifa sahihi
kuhusu masuala yanayowahusu na kuepuka uandishi wa habari zenye
kuhukumu.
Amesema
kisheria mtuhumiwa huwa hana hatia mpaka itakapothibitishwa na mahakama
kuwa ametenda kosa na kuongeza kuwa kukosekana kwa weledi katika
uandishi wa habari za mahakama huleta mkanganyiko miongoni mwa jamii
kuhusu ukweli na kuondoa imani ya watu kwa mahakama.
Ameongeza kuwa
baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa Vikitoa habari zisizo mpatia mtu
fursa na haki ya kujibu tuhuma huku vingine vikitoa taarifa nusunusu na
kushindwa kuwa na mwendelezo wa habari za mashauri mbalimbali
mahakamani.
Mhe.Chande
ameeleza kuwa waandishi wamejikita katika uandishi wa taarifa zenye
mvuto kwa jamii na kusahau nyingine walizo anza nazo jambo
linalosababisha wananchi kuachwa njia panda bila kupata taarifa za kina
kuhusu mwisho wa mambo yanayoanzishwa.
” Mimi sitaki
kuingilia utendaji wa kazi zenu za kila siku ila nachotaka kusema ni
kuweka msisitizo wa utoaji wa habari za mashauri mbalimbali mnayoanza
kuyaripoti kwa mwendelezo ili msiwachanganye wananchi” Amesisitiza.
Amewataka
waandishi wa habari kuandika habari sahihi na kuepuka upendeleo na
maslahi binafsi ili kulinda taaluma na imani katika jamii juu ya
utendaji wa vyombo vya habari.
Mhe. Chande
ametoa wito kwa waandishi wa habari kuepuka uandishi wa habari zilizojaa
chuki zinazoweza kuleta mgawanyiko katika jamii na kusisitiza habari za
kuisaidia jamii kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Kuhusu Mahakama
amesema itaendelea kuboresha huduma na miundombinu yake katika maeneo
yasiyofikiwa ili kuendelea kutoa haki kwa wakati pia kushirikiana na
waandishi wa habari wa ndani ili kuimarisha utendaji wao.
Aidha amevipongeza vyombo vya habari kwa ukomavu viliouonyesha wakati wa utoaji wa taarifa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Kwa upande wake
Rais wa Baraza la Habari Tanzania Mhe. Jaji Mstaafu Mhe.Thomas
Mihayo akizungumza kwa niaba ya Baraza hilo ametoa wito kwa waandishi wa
habari kuzingatia weledi katika uandishi wa habari za mahakama ili
kuepusha madhara katika jamii.
Amewataka waandishi kujikita zaidi katika uandishi wa habari zenye uhakika kuliko kuwa na taarifa zenye mlengo wa kuuza gazeti.
Amesema kuwepo
kwa mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania ni ishara
nzuri ya uboreshaji wa taaluma ya habari hasa uongezaji wa ushirikiano
katika kutekeleza majukumu ya kimahakama hapa nchini.
Amewataka
wanahabari kujifunza na kufuatilia miongozo na kufuatilia taarifa
mbalimbali zinazoweza kuboresha uandishi wao kwa kupata maneno sahihi ya
kimahakama.Amesema Semina hiyo itawasaidia waandishi wa habari kujenga
weledi katika uandishi wa habari za mahakama.
Ametoa
tahadhari kwa waandishi kuepuka uandishi wa habari zenye uchochezi ili
kuepuka kushtakiwa na jamii, kuepuka lugha za kishabiki na upendeleo.
Naye Meneja wa
Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Allan Lawa akizungumza kwa
niaba ya washiriki wa mafunzo hayo amewataka kuepuka kuandika habari
zinaonyesha upendeleo na kubainisha kuwa kuwa ipo haja kwa vyombo vya
habari kutenga maeneo madawati ya habari hizo
Tags
HABARI KITAIFA




