 |
| Uwekwaji Nyasi ukiendelea katika Uwanja wa Kaitaba leo hii. |
Taswira kamili
Uwanja huo umeanza kuwekwa nyasi rasmi leo na ndani ya siku 14
utamalizika na taratibu nyingine zitafuata na timu ya Kagera itaanza
kuutumia Uwanja huo. Uwanja huu sasa utakuwa umeongezeka katika viwanja
vilivyowekwa nyasi hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na uwanja wa uwanja wa
Uhuru uliopo Dar es Salaam, uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na uwanja
wa Gombani uliopo Pemba.
Taswira ya nyasi zenyewe za bandia zikiwa zimetandazwa katika
Uwanja huo wa Kaitaba uliopo Bukoba Mjini ambao hutumiwa na timu ya
Kagera Sugar ambayo kwa sasa inaendelea kutumia uwanja vya Ali Hassan
Mwinyi wa Tabora.
Katibu wa KRFA Salumu Umande Chama ambaye pia ni kiongozi kamati ya
Waamuzi nchini akizungumzia suala zima la uwanja huo wa Kaitaba na
waandishi wa habari Jumatatu 02 Novemba, 2015. Chama ameeleza kutokana
na kasi iliyopo na kama mafundi hawatakwama uwanja huo utamalizika ndani
ya wiki mbili tu.
 |
Na Faustine Ruta, Bukoba
Uwanja wa Kaitaba Bukoba umeanza kuwekwa nyasi bandia rasmi leo hii
Jumatatu 2 Novemba, 2015 na kutokana na maelezo ya wawekaji wa nyasi
hizo, wamesema utachukuwa muda wa siku 14 tu.
Wakaazi wa Mji wa Bukoba na vitongoji vyake sasa kuanza kushuhudia kipute live bila chenga katika uwanja huo wa Kaitaba.
Timu ya Kagera Sugar nayo inatarajiwa kurudi katika uwanja huo ambao
huutumia kama uwanja wao wa nyumbani lakini tangu msimu uliopita
wamekuwa wakitumia viwanja vingine kwa michezo yao ya nyumbani.
Uwanja wa Kaitaba unajengwa kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. |