9.39am:Vilevile aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya
raila Odinga ambaye ni rafiki mkubwa wa rais mteule John Pombe Magufuli
ni baadhi ya viongozi waliowasili mapema nchini Tanzania kwa sherehe
hiyo ya kihistoria. 9.35am:Miongoni mwa viongozi
wanaotarajiwa katika hafla hii ni pamoja na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
ambaye tayari ameondoka katika uwanja wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi
akiandamana na Mkewe bi. Margeret Kenyatta na anatarajiwa kuwasili
katika uwanja wa sherehe hizi wakati wowote kutoka sasa 9.30am:Gwaride
la kijeshi tayari limejiandaa vilivyo ikiwemo wanajeshi waliovalia sare
za rangi tofauti hapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 8:00 am Mataifa mbalimbali yamekuwa yakituma risala za pongezi kwa Tanzania na kwa Rais Mteule John Magufuli.
Wa kwanza kutuma risala za pongezi walikuwa ni:
Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Saharawi Mohammed Abdelaziz.
Katika
salamu zake kwa Rais Mteule Magufuli, Bw Kagame amesema: "Kufuatia
kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda
kukutumia Mheshimiwa salamu za dhati, pongezi na heri nyingi kwa niaba
yangu mwenyewe, Serikali yangu na wananchi wa Rwanda.”
Naye Rais
Abdelaziz amemwambia Rais Mteule Magufuli: “Sisi tuna uhakika kuwa chini
ya uongozi wako wa busara, Tanzania itaendelea kusonga mbele na kupata
maendeleo na ustawi mkubwa zaidi.” 7:10 am
Viongozi wa baadhi ya mataifa ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo
Jacob Zuma kutoka Afrika Kusini, Robert Mugabe kutoka Zimbabwe na
Filipe Nyusi wa Msumbiji. Mhubiri mashuhuri kutoka Tanzania TB Joshua
pia atahudhuria sherehe hiyo. 7:00 am Watumbuizaji wanaotarajiwa kutumbuiza wakati wa sherehe walifika uwanjani mapema na ala zao.
6:45 am Uwanja umeanza kujaa watu. Wengi wa
waliofika mapema wanafurahisha kujipiga, kupigana na kupigwa pichwa
kuweka kama kumbukumbu za siku hii.
6:30 am Uwanja wa Uhuru umepambwa ukapambika
6:30 am Sherehe ya kumuapisha Bw Magufuli inafanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
6:00 am. HABARI YA ASUBUHI?
Rais
Mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli anaapishwa leo kuwa rais wa
awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa
mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 25.
Bw Magufuli alipata asilimia 58.46 ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania