BANDA MEDIA BLOG

Rais Magufuli afanya Ziara ya Kushtukiza Hazina.

 Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika makao makuu ya Wizara ya Fedha(HAZINA) kwa ziara ya kushtukiza leo
mchana.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Servacius Likwelile.Rais Magufuli alitembelea na kukagua ofisi zote wizarani hapo na kisha kuongea na viongozi waandamizi.
 Rais Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Wizarani hapo ambapo alitoa maagizo ya kuziba mianya ya wakwepa kodi.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na wafanyakazi wawili wa Wizara ya Fedha ambao ni walemavu Bwana Fundi Maruma na Frank Mkyama wakati Rais alipofanya ziara ya kushtukiza wizarani hapo leo.(picha na Freddy Maro)

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG