 |
Kijana mmoja wa Syria ambaye
kutoweka kwake hospitalini mjini Belgrade akiwa katika kambi ya
wakimbizi barani Ulaya kulizua hisia kali miongoni mwa mitandao ya
kijamii ameunganishwa tena na wazazi wake nchini Ujerumani.
Mwandishi
wa BBC John Sweeny aliyeongoza utafutaji wa Azam mwenye umri wa miaka
mitano alichapisha habari hizo katika mtandao wa twitter.
Azama alisafiri mbele ya wazazi wake na mjombaake na alijeruhiwa wakati wa safari hiyo.
Habari
yake ilianzisha kampeni katika mitandao ya kijamii yenye alama ya reli
FindAzam.Azama hakuwa pekee katika familia hiyo aliyejeruhiwa wakati wa
safari hiyo kutoka Syria kuelekea Ulaya. |

Kukutanishwa kwake na familia yake siku ya Alhamisi kulifanyika
katika hopositali moja ya Ujerumani ambapo babaake anatibiwa mguu wake
uliovunjika wakati wa safari hiyo kupitia Ugiriki.
John Sweeney alikutana na Azam huko Serbia mnamo mwezi Septemba alipokuwa akitengeza makala kuhusu wakimbizi hao.
Mvulana
huyo alikuwa akilia na uchungu mwingi kwa sababu gari moja lilimkanyaga
alipokuwa usingizini ,na hivyobasi kuvunja taya lake.Lakini kabla ya
kukamilisha matibabu mjini Belgrade,Azam alipotea na mjombaake
 |
| Picha za Azam zilizosambazwa kwenye mitandao ili kumtafuta |
Kwa kipindi cha BBC Newsnight,Sweeney aliitafuta njia iliochukuliwa
na wakimbizi hao ambayo Azam na mjombaake walitumia,akisafiri kutoka
Serbia hadi Hamburg ambapo mtoto huyo hatimaye alipatikana na kundi moja
la waandishi wa BBC baada ya usakaji mrefu uliohusisha utumizi wa
mtandao wa kijamii.
Mjombaake ameiambia BBC kwamba kigae kiliingia
katika jicho la Azam wakati wa mashambulizi mjini Damascus na aliagizwa
na wazazi wa mvulana huyo kuelekea naye haraka Ujerumani ili kutibiwa
CHANZO BBC