BANDA MEDIA BLOG

TIMU YA WATAALAMU WA AFYA YAFANYA MAFUNZO YA UKAGUZI WA VITENDO BANDARI

NA RAYMOND MUSHUMBUSI – MAELEZO
 Timu ya wataalamu wa afya kutoka vituo vya Afya, Bandari, Viwanja vya Ndege na mipaka ya nchi kavu ambayo imejumuisha maafisa wa afya na mazingira, madaktari na wauguzi kutoka Tanzania bara na Zanzibar imefanya mafunzo ya vitendo ya ukaguzi wa meli ndani ya bandari ya Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mratibu wa  Vituo vya Afya Bandari na Viwanja vya Ndege Bw. Remidius Kakulu amesema wataalamu hawa wapo katika mafunzo ya vitendo yanayoratibiwa na kuendeshwa na wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ikishilikiana na Shirika la Afya  Duniani (WHO).
Amesema malengo ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo  wakaguzi wa vyombo vya usafiri zikiwemo meli na ndege na kutoa vyeti vya usafi vya kimataifa kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo hivyo. Mafunzo haya yatawezesha kuandaa vituo vyetu vya ukaguzi kwa viwango vya kimataifa kwa mujibu wa kanuni za afya za kimataifa za mwaka 2005.
Aidha katika ukaguzi huo ulifanikisha kukagua meli nne(4) za mizigo na magari na kufanikiwa kukagua sehemu kumi na tatu(13) zikiwemo sehemu za kulala mabaharia(Quarters),sehemu za jikoni na store za kuhifadhia vyakula, utunzajia na udhibiti wa dawa ( Medical facilities),sehemu za kuogelea( swimming pools), udhibiti wa taka ngumu na taka zitokanazo na mabaki ya madawa( medical wastes), upatikanaji wa maji safi na salama,udhibiti wa maji taka,udhibiti wa umwagiliaji wa maji yanayosaidia balance ya meli ( Ballast water) na maeneo mengine ambayo yanaweza kuhatarisha afya ya binadamu na mazingira.
Mmoja wa maafisa aliyeshiriki mafunzo hayo Bw. Onesmo Masta Kitange Afisa Afya Mkuu Mazingira kutoka Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  amesema mafunzo hayo yamewasaidia kupata utaalamu zaidi na kujiamini katika kazi zao za ukaguzi katika vyombo vya usafiri licha ya changamoto mbalimbali.
Naye Bi Eliengera Mghase ambaye ni Afisa Afya Mwandamizi Bandari  amesema mafunzo hayo ya siku sita (6), kwa mafunzo ya siku tano (5) ya darasani na siku moja kwa vitendo ambayo yamewawezesha kupata utaalamu zaidi katika kazi zao za ukaguzi wa vyombo vya usafiri vya majini na nchi kavu.
Mafunzo hayo yalijumuisha makundi mawili tofauti likiwemo kundi la kwaqnza lilifanya mafunzo kwa vitendo kuanzia tarehe 3/11/2015 hadi tarehe 8/11/2015 na kundi la pili lililomalizia kutoka tarehe 10/11/2015 hadi tarehe 13/11/2015amabayo yamewasaidi kuongeza ufanisi kutoka ukaguzi wa sehemu tatu(3)  tu katika meli mpaka kufikia sehemu kumi na tatu (13) hivyo kuongeza weledi kwenye kazi zao hasa kudhibiti mapungufu yanayojiyokeza.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG