Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akichangia majadiliano kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Ofisi ya Rais wa Baraza Kuu, alipendekeza kupitiwa kwa bajeti ya Ofisi ya Rais wa Baraza hilo, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha kwamba ofisi hiyo inakuwa na raslimali fedha na watumishi wa kutosha kulingana na majukumu yake. Pia akasema Tanzania inaunga hoja wanawake wenye uwezo kupewa nafasi ya kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa, Bw. Mogens Lykketoft akizungumza kabla ya kumpa nafasi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, wakati Baraza hilo lilipokutana pamoja na mambo mengine kujadili ajenda ya uboreshwaji wa utendaji kazi wa Ofisi ya Rais wa Baraza Kuu. Majadiliano hayo yalitawaliwa na tuhuma nzito za rushwa zinazomkabili aliyekuwa Rais wa Baraza Kuu la 68 la Umoja wa Mataifa. Bw. John Ashe. Akizungumzia tuhuma hizo, Ban Ki Moon amesema vitendo vya rushwa haviwezi kuvumiliwa ndani ya chombo hicho na kwamba tuhuma hizo zimeathiri taswira na heshima ya Umoja wa Mataifa.
Tags
KIMATAIFA
