BANDA MEDIA BLOG

STAND UTD YADAIWA ZAIDI YA 800,000 NA ANAYEWACHEMSHIA MAJI YA KUNYWA


Kikosi cha Stand United kilichoanza dhidi ya Simba
Timu ya Stand United imeendelea kujiweka pabaya baada ya mtu mwingine kuibuka na kusema anaidai Stand pesa kutokana na huduma ya kuchemsha maji ya kunywa kwa ajili ya wachezaji wa timu hiyo.
Mariam Rajab maarufu kama ‘mama mchungaji’ amedai kuwa amekua akitoa huduma hiyo kwenye klabu ya Stand United tangu kuanzishwa kwa timu hiyo iliyoanza kushiriki daraja la nne hadi daraja la kwanza ambapo huko alikuwa analipwa pesa yake. Lakini tatizo lilianza baada ya timu hiyo kupanda kucheza ligi kuu.
“Timu ya Stand United naidai pesa, nilikuwa nikitoa huduma ya maji katika timu ya Stand kuwahudumia wachezaji. Waliniomba niwachemshie maji halafu niwauzie. Nimefanya hivyo tangu timu ilivyoanzishwa tangu ikiwa ligi daraja la nne mpaka ligi daraja la kwanza tulikuwa tunaenda sawa pesa yangu walikuwa wananipa”, amesema mama mchungaji.
“Walipoingia ligi kuu wakaniambia niendelee kuwachemshia maji lakini wakasema pesa yangu watanipa pindi watakapopata pesa za udhamini kutoka Vodacom tutakupa pesa yako wewe tupigie tu hesabu unatudai kiasi gani”.
“Mimi nilivumilia nikawa nafanya hiyo kazi nachemsha maji napeleka tunaandikiana hesabu hadi ligi ikaanza Stand ikacheza mechi ya kwanza na Ndanda. Nikaulizia pesa yangu wakaniambia nisubiri wamalize mechi  lakini baada ya mechi nikaambiwa mambo bado hayajakaa sawa lakini niendelee kutoa huduma. Mpaka msimu ukamalizika sikupewa hela yangu”.
“Wakaniambia mama wewe mwenyewe unaona mambo magumu, na kunakipindi walikuwa wanaomba niwaazime pesa yangu huku wakiniambia niwe mvumilivu kwasababu kuna mdhamini wamempata wa ACACIA mambo yatakuwa mazuri nipige hesabu ya pesa zote ninazowadai wambo yatakuwa sawa”.
“Tukaanza msimu wa pili wakaniambia endelea kutoa huduma tutakapoanza mechi ya kwanza tutakulipa pesa yako kwasababu sasahivi timu inahali nzuri, na mimi kweli nikaona amepatikana mfadhili mkubwa pesa watakuwanazo nikaendelea kutoa huduma”.
“Ilipofika tarehe 23/8/2015 wakasitisha huduma bila kunipa pesa yangu wakaniambia nisubiri pesa za gate collection tutakapocheza na Azam tutakulipa pesa yako nikawaambia sawa nitavumilia. Mechi ikapita wakaniambia pesa hakuna, zimezuiliwa”.
“Kiasi ninachowadai ni shilingi 880,000 mpaka sasahivi lakini viongozi nikiwafata wananiambia yaleyale nisubiri wakae kikao, nimezungumza na mwenyekiti kaniambia pesa hakuna wapo kwenye hali mbaya lakini ukiangalia sasahivi timu inahali nzuri  na pesa wanazo, naomba  wadu wote popote pale wanisaidie nipate haki yangu ikiwezekana hata Malinzi na Wambura wanisaidie niweze kupewa haki yangu”.
Timu ya Stand United imeingia kwenye mgogoro baada ya kupata pesa za udhamini kutoka kampuni ya uchimbaji madini. Hivi karibuni aliyekuwa Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Muhibu Kanu alilalamika kutopewa malipo yake ambayo anadai kutoka kwenye klabu hiyo.
Inasemekana Stand United imeshatumia zaidi ya nusu ya shilingi bilioni moja ambayo wamepewa na ACASIA kwa ajili ya msimu huu ikiwa hata mzunguko wa kwanza wa ligi bado haujamalizika.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG