Stephen Curry alifunga pointi 46, huku 21 zikiwa katika robo ya
kwanza, na kuisadia Golden State Warriors kuboresha rekodi yake ya
ushindi kuwa 10-0 katika ushindi wa 129-116 dhidi ya Minnesota
Timberwolves Alhamisi usiku.
Draymond Green alikuwa na pointi 23, pasi 12 na rebounds8 kwa Warriors, ambao wanakuwa ni mabingwa watetezi wa nne kuanza msimu na angalau ushindi mara 10 mfululizo pasi na kupoteza. Curry alipata mitupo 15 kati ya 25aliyojaribu, ikiwa ni pamoja na mitupo 8 kati ya 13 kutoka katika eneo la point 3.
Karl- Anthony Towns alimaliza na pointi 17 na 11 rebounds na Andrew Wiggins alifunga pointi 19 kwa Minnesota Timberwolves ( 4-4 ) , ambao wamepoteza michezo yote minne ya nyumbani msimu huu.
Celtics katika misimu ya 1957-1958 na 1964-1965 na Chicago Bulls katika msimu wa 1996-1997 zinakuwa timu nyingine pekee ambazo zilikuwa mabingwa watetezi katika NBA na kuweza kuanza msimu kwa ushindi mara 10 mfululizo.
Mwaka jana Russell Westbrook aliongoza NBA kwa kufunga point 20 katika robo moja mara nne tofauti. Mpaka sasa Stephen Curry tayari ana robo nne ambazo ameweza kufunga point 20 au zaidi na ni katika michezo 10 pekee.

Tags
MICHEZO KIMATAIFA