Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi leo Jumamosi Desemba 5,
2015 alihudhuria mkutano wa Halmashauri ya CCM tawi la DMV ikiwa ni moja
ya ziara zake anazotarajiwa kuzifanya kutembelea matawi ya vyama vya
siasa nchiMarekani yenye lengo la kudumisha mshikamano na ushirikiano wa
Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao.
Akiongea kwenye mkutano wa
Halmashauri ya CCM DMV Mhe. Wilson Masilingi amesema lengo kuu ni kuwa
karibu na vyama vya siasa kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano ndani
ya Jumuiya za Watanzania nchini Marekani na pia kuvitambua kama sehemu
na sura ya Diaspora na kutoa wito kwa Watanzania waishio Marekani
kuelekeza nguvu katika kuwekeza nyumbani bila kujali ufuasi wa chama
unachoamini au kushabikia, wote ni Watanzania.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi
aliiomba Halmashauri hiyo ya CCM DMV kusaidia katika maendeleo ya
Tanzania kwa kupanua wigo wao pamoja na kwamba lengo lao ni siasa na
siasa ni sehemu ya maisha ya jamii na maendeleo ya jamii yanategemea
siasa, kwa hiyo basi mnaposikia kuna muwekezaji yupo tayari kuwekeza
Tanzania msisite Ubalozi upo wazi na utafanya kila liwezekanalo
kuhakikisha muwekezaji huyo hapati vikwazo vyovyote.
Mwisho Balozi Wilson Masilingi
aliwashukuru Watanzania kwa kuwa mabalozi wazuri nchini Marekani na
kuwaasa kuishi kwa kufuata misingi na sheria za nchi ya Marekani.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea jambo na mwenyekiti wa tawi
CCM DMV Bwn. George Sebo kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV siku
ya Jumamosi Desemba 5, 2015 mkutano uliofanyika Hampton Inn, College
Park, Maryland. Picha na Kwanza Production/Vijimambo BlogMkutano ulianza kwa sala na kuwakumbuka wote waliotangulia mbele ya haki.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea machache kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM DMV kilichofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn, College Park, Maryland.
| Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea machache kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM DMV |
| Bwn. John Mbatta katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi. |
Given katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
|
| Aunty Grace Sebo katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi |
| Grace Mlingi katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi. |
| Mzee Joel katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi. |
| Katibu wa CCM DMV Bi.Jesca Mushala katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi. |
| Picha ya pamoja. |
Tags
HABARI KITAIFA