Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akizungumza
na washiriki wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi wa Mkataba wa Idara ya
Huduma kwa Wakimbizi(hawapo pichani),wakati alipofungua mafunzo hayo
yenye lengo la kuwajengea uwezo watumishi wapya, katika ukumbi wa
mikutano wizarani hapo,jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Numbilya Mpolo.
Washiriki
wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa
Wakimbizi, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani), wakati alipofungua mafunzo hayo
katika ukumbi wa mikutano wizarani hapo,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa, akizungumza na washiriki wa Mafunzo ya
awali kwa Watumishi wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi(hawapo
pichani),kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Utawala na
Usimamizi wa Idara ya Wakimbizi, Deusdedit Masusu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watatu kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, muda mfupi baada ya kufungua mafunzo hayo katika ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam wanne kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa na wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Numbilya Mpolo .(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,MOHA)
Tags
HABARI KITAIFA