![]() |
![]() |
| Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu Fak akifunga mafunzo ya walimu wa michezo wa Skuli katika Skuli ya Elimu Mbadala Rahaaleo Mjini Zanzibar. |
![]() |
| Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu Faki akiwakabidhi vyeti washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Kamati ya TOC katika Ukumbi wa Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Zanzibar. |
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar
Idara ya ya Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar imeshauriwa kuwaandalia michezo nje ya nchi walimu wa
michezo wa skuli kwa lengo la kujipatia taaluma zaidi na kukukuza
mechezo nchini ,
Hayo yameelezwa huko Rahaleo
katika Ukumbi wa Elimu Mbadala na Watu wazima na Mkurugenzi Idaraya hiyo
Zanzibar Mashavu Faki wakati akifunga mafunzo yalioandaliwa na Kamati
ya Olimpiki Tanzania (TOC) yaliyofunguliwa tarehe 1 mwezi huu.
Amesema iwapo walimu wa michezo
watapatiwa mafunzo zaidi nje ya nchi wataweza kuwasomesha wanafunzi wao
wa skuli na kuinua sekta ya michezo Zanzibar.
Mkurugenzi Mashavu amesema katika
mwaka 2013 kulifanywa utafiti wa kimchezo na kuonekana kuwa nchi
zinazoimarisha michezo maskulini ndizo zinazofanya vizuri zaidi katika
masomo yao.
Aidha amesema michezo huimarisha
afya, kujenga upendo, udugu na uzalendo katika jamii hivyo hakuna budi
kuendelezwa kwa manufaa ya wanamichezo wenyewe na Taifa kwa jumla.
Sambmba na hayo Mkurugenzi huyo
amewashauri waalimu waliopata mafunzo hayo kwa kushirikiana na Idara
husika kuandaa mafunzo kila baada ya miezi mitatu.
Nae mkufunzi wa mafunzo hayo
Suleiman Mahamoud Jabir amewataka washiriki wa mafunzo hayo kujenga moyo
wa kujitolea kwani katika kufundisha mara nyingi hujitokeza matatizo
mengi.
Kwa upande wao waalimu waliopata
mafuzo hayo Mussa Abdulrab na Arafa Talib Omar wamesema wamejifunza
mambo mengi wasioyajua na kuahidi kuwa watayafanyia kazi.
Mafunzo hayo ya siku tano ya walimu wa michezo wa skuli mbali mbali za Zanzibar yameandaliwa na Kamati Tanzania.
Tags
MICHEZO


