Taarifa kwa vyombo vya habari
Wizara ya afya kuanzia leo 24
Desemba 2015 imepiga marufuku matangazo yote yanayohusu tiba asili na
tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Kwa wale wenye vibali wanatakiwa
kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba Asili na
Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.
Utoaji wa elimu ya afya kwa umme
unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo
vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi hapo utaratibu
mwingine utakapotangazwa.
Watoa huduma za tiba asili na tiba
mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza nyaraka zote
muhimu ndani ya wiki mbili kuanzia leo Desemba 2015. Baadhi ya nyaraka
hizo ni zile zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za
kumiliki mashine zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili
na tiba mbadala
Baraza la Tiba Asili na Tiba
Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia leo 24 Desemba
2015, lipitie nyaraka zote zikapowasilishwa zinazohusu usajili wa watoa
huduma, usajili wa vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za
asili na dawa za tiba mbadala, usajili wa dawa zote zinazotumika katika
huduma hizo na usajili wa mashine zote zinazotumika katika huduma za
tiba asili na tiba mbadala.
Taarifa
hii imetolewa na Dismas Lyassa kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangala na
kusainiwa na M.O John, Kaimu Katibu Mkuu
Tags
HABARI KITAIFA