Timu za Azam FC, Simba SC, Yanga
zimeungana na timu zingine saba kufuzu kwa hatua ya 16 Bora ya michuano
ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa nne
utakaochezwa mwishoni mwa mwezi Februari, huku michezo mine ikichezwa
leo katika viwanja mbalimbali nchini.
Jumla ya michezo 10 mpaka sasa
imeshachezwa na timu kumi kujikatia tiketi ya kucheza mzunguko wa nne,
ambao utazikutanisha jumla ya timu 16 mwezi ujao kusaka timu nane
zitakazosonga mbele hatua ya nane bora (Robo Fainali).
Timu zilizofuzu hatua ya 16 bora
mpaka sasa ni Azam FC, JKT Mlale, Mwadui FC, Ndanda FC, Panone FC, Rhino
Rangers, Simba SC, Tanzania Prisons, Toto Africans na Young Africans.
Leo michezo minne itachezwa,
Mtibwa Sugar v Abajalo (Jamhuri – Morogoro), Geita Gold v Mgambo
Shooting (Nyankumbu – Geita), Lipuli FC v JKT Ruvu (Wambi – Mafinga), na
African Sports v Coastal Union (Mkwakwani – Tanga).
Bingwa wa michuano ya Kombe la
Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mwaka huu, ataiwakilisha
Tanzania mwaka 2017 kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika
(CAF-CC)
Tags
MICHEZO