![]() |
| Mbwana na Kalou |
![]() |
| Mbwana akishangilia moja ya Goli lake pamoja na waenzake |
Samatta amesema alikuwa anahisi anakuwa chizi kutokana na furaha aliyokuwa nayo baada ya dili hilo kukamilika ambalo limeifanya ndoto yake ya siku nyingi ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya kukamilika.
“Nilikuwa nahisi nakuwa chizi kutokana na furaha niliyokuwa nayo. Ukiwa na ndoto halafu unaona ndoto yako inakuwa kweli, na kilichotokea ni kama kuna giza mbele na unashindwa kuona hicho ndicho kilichotokea kwangu”, alisema Samatta.
“Naiheshimu TP Mazembe, namuheshimu Rais wa Mazembe Moise Katumbi. Sitaki kusababisha matatizo yoyote na wao kwasababu wamenichukua tangu nikiwa mdogo na kunilea. Nimekulia Mazembe nikisubiri wakati muafaka hadi klabu yangu ifikie makubaliano na klabu inayonihitaji”.
Samatta amesaini kandarasi ya miaka minne (4) kukitumikia kikosi cha Genk ambapo anatarajia kuhudumu kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2020.
Cheki Vieo hapa Samatta akifunguka kuhusu kukamilika kwa dili lake la kujiunga na klabu ya Genk.
Tags
MICHEZO KITAIFA

