Na Rabi Hume, Modewjiblog
Miss
Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu amemaliza mwaka 2015 kwa kutembelea
kituo Nunge ambacho ni makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza kilichopo
Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Hoyce
ambaye amekuwa akisaidia watu wa aina mbalimbali wenye matatizo ikiwa
ni kama moja ya kazi wanazofanya mamiss kwa jamii pia kupitia kipindi
chake cha Mimi na Tanzania ambacho kimekuwa kikisaidia watu mbalimbali
na katika halfa hiyo aliongozana na watu wake wa karibu ikiwepo kamati
ya Miss Tanzania.
Katika
halfa hiyo iliyodhaminiwa na Malaika Beach, Hoyce baada ya kuwasili
kituoni hapo yeye na timu nzima aliyoongozana nayo walifanya shughuli za
kijamii katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika
makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza waliopo kituoni kwa kupulizia
dawa za kuulia wadudu katika nyumba zao, kugawa dawa za mbu, maji, juice
na biskuti na baadae wakapata chakula cha pamoja na wazee na walemavu
wasiojiweza.
Akizungumzia
halfa hiyo ya kufunga mwaka, Hoyce Temu alisema kumekuwepo na
kusahaulika kwa makundi ya watu wasiojiweza na jinsi muda unavyokwenda
wanazidi kusahaulika na jamii inayowazunguka.
Alisema
yeye kama Miss Tanzania ana wajibu wa kujitoa kuwasaidia watu wa aina
hiyo na amekuwa akifanya maeneo mengi kwa kujumuika nao kwa kuwapa
msaada na kuwafariji kwani nao wana thamani kama binadamu wengine.
“Kadri
inavyokwenda kumalizika karne ya 21 kunazidi kuongezeka kwa makundi ya
wasiojiweza na mimi kama Miss Tanzania nimeamua kujitoa kwa kusaidia
makundi haya kwani ni wajibu wetu na tukumbuke na sisi tunaelekea huko,” alisema Hoyce.
Aidha
Hoyce alitoa ushauri kwa mamiss wenzake kuwa wanatakiwa kuisaidia jamii
kwa kutumia fursa walizonazo mbele ya jamii kwa kutoa misaada kwa
makundi ya aina mbalimbali.
Alisema
kazi ya kusaidia jamii siyo ya serikali pekee na wao kama mamiss na
watu wenye uwezo kwa ujumla wana wajibu wa kusaidia na sio kutazama
mijini pekee kutokana na kundi kubwa la wasiojiweza kuwa vijijini.
“Sio
swala la serikali pekee … ukichaguliwa kuwa mrembo unakuwa na malengo
ambayo umeyaweka hivyo watumie umaarufu, sura zao na sauti kufikia watu
wa aina mbalimbali ambao wanahitaji msaada, ” Na sio wazee pekee,
65% ya nchi yetu ni vijana na 20% wanajihusisha na kutumia madawa ya
aina mbalimbali hivyo wanaweza kuwatembelea na kutoa elimu juu ya athari
za utumiaji wa madawa hayo,” alisema Hoyce.
Nae
Mkurugenzi wa Lino International Agency, ambayo ndiyo waandaji wa
shindano la Miss Tanzania, Hashimu Lundenga alimtaja Hoyce kama Miss
bora kuwahi kutokea tangu walipoanzisha shindano la Miss Tanzania mwaka
1994.
Alisema
mamiss wengi wamekuwa wakiisaidia jamii lakini Hoyce amekuwa akijitoa
zaidi kuliko wengine na kufanya shindano hilo kuonekana kuwa na faida
mbele ya jamii.
“Naomba
niseme ukweli Hoyce anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa haijawahi kutokea
miss aliyejitoa kusaidia jamii kama yeye na wapo wengine wanasaidia ila
Hoyce amekuwa mstari wa mbele kwa hilo tunampongeza na tunamwomba azidi
kuwa hivyo,” alisema Lundenga.
Kwa
upande wa Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi amemshukuru
Hoyce kwa upendo amekuwa nao kwa kituo hicho ambacho awali aliwahi
kukitembelea 2006 akiwa na marehemu Amina Chifupa na kumtaka kuzidi kuwa
na moyo huo kwa jamii inayomzunguka.
Mgedzi
pia alizungumzia changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na kutokuwepo
kwa uzio hivyo kutokuwa na hali ya usalama, kuvamiwa kwa eneo hilo na
wananchi ambalo lina hekali 50.8 na tayari asilimia 50 imevamiwa na
tayari taarifa ipo wizarani na wanashughulikia na zingine ndogo ndogo
Hoyce akiahidi kuwasaidia.
Nae
mmoja wa washiriki aliyeongozana na Hoyce, Tausi Mwenda alisema kuwa
amejifunza mambo mengi kupitia halfa hiyo aliyoifanya Hoyce na
kuwashauri watu wa aina mbalimbali kuwa na moyo wa kujitoa kusaidia
jamii kama anavyofanya Hoyce.
Tags
HABARI KITAIFA