Waziri
wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,Mh.Mwigulu Lameck Nchemba akisikiliza kero za
wadau wa machinjio ya Vingunguti usiku huu wa January 1/01/2016.
Mwigulu Nchemba akishuhudia Ng’ombe aliyetayari kwa taratibu za kuchinjwa kwaajili ya kitoweo.
Mbuzi
wakiwa tayari kwaajili ya kuchinjwa kwenye machinjio hayo ya
Vingunguti.Mbuzi hawa asilimia kubwa wanatoka mnada wa pugu ambao Ushuru
wake unakusanywa na serikali kuu.
Waziri Mwigulu Nchemba akikagua maeneo ya machinjio hayo usiku huu.
Mwigulu
Nchemba akitoa maagizo kwa uongozi wa Machinjio ya Vingunguti kukutana
kesho saa 2:00 asubuhi kwa wahusika wote wenye dhamana na Machinjio
hayo,Mkutano utafanyika eneo la Machinjio hayo.
…………………………………………………………………
Katika
hatua ya kushitukiza,Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu
Nchemba amefanya ukaguzi wa Machinjio ya Vingunguti usiku huu.
Mh.Mwigulu
Nchemba amefika kwenye Machinjio hayo usiku huu ilikushuhudia Mifugo
ikiandaliwa kwaajili ya kitoweo cha wananchi.Uchinjaji wa Ng’ombe na
Mbuzi katika machinjio haya hufanyika nyakati za Usiku kuanzia saa 4
hadi 10 alfajiri.
Mbali
na kusikiliza kero na maoni ya wananchi kuhusu uendeshwaji wa Machinjio
hayo,Mwigulu Nchemba ameshuhudia utafunwaji wa kodi ya serikali
inayokusanywa kwenye mnada wa pugu.
Utafunwaji
huo unatokana na uandikaji wa kibali cha mifugo michache kuja
Machinjioni ili hali mifugo Zaidi huingizwa machinjioni bila
kibali.Matharani hii leo Mh.Waziri ameshuhudia Ng’ombe waliotoka mnada
wa pugu ambao wameshalipiwa kodi wakiwa 1450 lakini kibali chake
kimeandikwa Ng’ombe 300 tu.Inamana kuna ng’ombe 1150 wamelipiwa ushuru
lakini machinjioni kimeletwa kibali cha ng’ombe 300 wakati kwa
kuwahesabu ng’ombe hao wanazidi 1000.
Kutokana
na hali hiyo,Mh.Waziri ameagiza wahusika wote kufika kesho kwenye
mkutano wa asubuhi kwaajili ya hatua stahiki kuchukuliwa,Mwigulu
amesisitiza kuwa kwa mtu yeyote mwenye dhamana na kusimamia sekta ya
kilimo,Mifugo na Uvuvi afanya kwa mujibu wa sharia,vinginevyo hakutakuwa
na huruma kwa wanaohujumu.
Tags
HABARI KITAIFA