BANDA MEDIA BLOG

LUIS SUAREZ AMEPACHIKA MABAO MATATU WAKATI BARCELONA IKIFANYA MAUAJI

Luis Suarez amepachika mabao matatu yaani hat-trick wakati Barcelona ikipambana kujaribu kutetea taji la La Liga kwa kuitundika Athletic Bilbao iliyokuwa na wachezaji 10 kwa mabo 6-0.

Bilbao walijikuta wakimpoteza golikipa wao Gorka Iraizoz aliyetolewa nje mapema kwa kumuangusha Suarez na kisha Lionel Messi kufunga kwa mkwaju wa penati.

Neymar alipachika bao la pili kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika, huku Suarez na Ivan Rakitic wakifanya matokeo kuwa 4-0 katika kipindi cha pili. Suarez alifunga bao la tano na la sita baadae.
                                                                 Lionel Messi akijipinda kupiga shuti 
                                        Luis Suarez akipiga shuti la mpira wa kuzungusha

Matokeo mengine ya La Liga Valencia 2 - 2 Rayo Vallecano, Real Madrid 5 - 1 Sporting de Gijón,  Getafe 3 - 1 Espanyol na Las Palmas 0 - 3 Atl Madrid.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG