Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura kabla ya
mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 13,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine
Mahiga (kulia) akizungumza na Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene
Kayihura walipokutana Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam
Januari 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura Ofisini
kwake jijini Dar es salaam Januari 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa
amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene
Kayihura. Ambapo amemuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na
Rwanda.
Akizungumza na Balozi Kayihura
jana ,(jumatano 13, 2016) ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es salaam,
Waziri Mkuu amemshukuru Balozi huyo kwa kumtembelea na ameahidi kuwa
Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano ulipo baina ya nchi hizi
mbili.
“Nia yetu ni kushirikiana kwa
pamoja kwa kuunganisha wafanyabiashara wetu, kwa kutumia Bandari ya Dar
es salaam na reli ya kati, ambayo tutajenga kwa kiwango cha kisasa
‘standard gauge’ ili ziweze kubeba mizigo mingi na kwenda mwendo wa
kasi” alisema Waziri Mkuu.
Kwa upande wake, Balozi wa
Rwanda, Kayihura amesema Tanzania na Rwanda ni nchi marafiki na
zinafanyakazi wa pamoja, Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania
kikanda na kimataifa.
“Tunatumia Bandari ya Dar es
salaam na Mombasa, tunashukuru kwa namna ambavyo mnaboresha Bandari ya
Dar es Salaam, kwani Rwanda inafaidika pia kwa vile mizigo yetu mingi
karibu asilimia 75 husafirishwa kupitia bandari hii” alisema Balozi
Kayihura
Tags
HABARI KITAIFA