Uongozi
wa Studio ya Muziki ya The Industry iliyoko chini ya Wanamuziki
Producer Nahreel na Aika Marealle unapenda kuchukua Nafasi hii
kuwatangazia Umma Kuwa kuanzia Tarehe 14 January 2016 Wamemuingiza
Msanii mpya wa Kike aitwaye Rosa Ree, Rose Ree ni muimbaji wa Muziki
aina ya Rap ambae kazi zake zitaanza kusikika/Kuonekana siku si nyingi
kuanzia sasa katika Redio Mbali mbali na TV Stations za Tanzania na nje
ya nchi.
Kama wasikilizaji na watazamani
tunaomba Kumuunga mkono Msanii huyu mpya Kwani tuna uhakika
hatawaangusha katika kuwaletea burudani Katika Masikio na macho yenu
pindi kazi zake zitakapoanza kutolewa hivi karibuni.
The Industry ni studio na
kampuni ya muziki ambayo ipo chini ya kundi la music lenye Mafanikio
makubwa la Navy Kenzo ikisimamiwa na Producer Nahreel na msaidizi wake
Aika Marealle
Wasanii Baadhi Waliokwisha
fanya kazi na Studio ya The Industry mpaka sasa toka kuanzishwa kwake
hivi karibuni ni Diamond Platnumz na wimbo wake wa Nana, Nikki wa Pili
na wimbo wa Baba Swalehe, Joh Makini na nyimbo zake kama Don’t Bother na
nusu nusu.
Tags
KIBURUDANI