Naibu Waziri Fedha na Mipango
Mhe. Dkt Ashatu Kijaji akifanya mazungumzo na dereva wa lori la mafuta
(hayumo pichani) mara alipowasili forodha ya Tunduma.
Naibu Waziri Fedha na Mipango
Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (kushoto) akikagua nyaraka za mizigo kutoka kwa
Bw. Baraka Lwesya (katikati) ambaye ni wakala kutoka kampuni ya Oceanair
Freight L.t.d. Kulia ni Katibu wa Naibu Waziri Fedha na Mipango na
Mchumi Bw. Moses Dulle.
Naibu Waziri Fedha na Mipango
Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (kushoto) akikagua nyaraka za mizigo kutoka kwa
Bw. Baraka Lwesya (katikati) ambaye ni wakala kutoka kampuni ya Oceanair
Freight L.t.d. Kulia ni Katibu wa Naibu Waziri Fedha na Mipango na
Mchumi Bw. Moses Dulle.
Naibu Waziri Fedha na Mipango
Mhe. Dkt Ashatu Kijaji akiwasikiliza baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania, Forodha ya Tunduma, Mbeya.
Naibu Waziri Fedha na Mipango
Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (katikati) akimsikiliza kwa makini Kaimu Meneja
Msaidizi wa Forodha ya Tunduma Bw. Majaliwa Ndungutu (kulia) na kushoto
ni Katibu wa Naibu Waziri Fedha na Mipango na Mchumi Bw. Moses Dulle
akifuatilia majadiliano hayo katika moja ya ofisi za Forodha Tunduma.
Picha na Eva Valerian– Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango.
…………………………………………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji atembelea forodha ya Tunduma na kujionea
utendaji kazi unavyofanyika pamoja na changamoto zinazowakabili.
Akiongea na Kaimu Meneja Msaidizi
wa Forodha ya Tunduma Bw. Majaliwa Ndungutu, Mhe. Dkt Kijaji alisema
Mamlaka ya mapato Tanzania ina wajibu wa kukusanya mapato ipasavyo ili
nchi iweze kusonga mbele.
Katika kuelezea majukumu ya
Forodha ya Tunduma Bw. Majaliwa alisema kuwa kazi kubwa wanayoifanya ni
kuwezesha mizigo inayosafirishwa kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda
nchi ambazo ni (land locked country) kwa kuzifanyia ukaguzi na
kuhakikisha kinachosafirishwa ndicho kilichopo kwenye makontena
kulingana na nyaraka za mizigo husika.
Pamoja na jukumu hilo Bw.
Majaliwa aliongeza kuwa kazi nyingine wanayoifanya ni kusafirisha mizigo
ambayo inazalishwa hapa nchini na kupelekwa nchi za nje.
“Ili kuhakikisha kuwa mizigo
inayosafirishwa inafika salama, lazima mizigo isafirishwe kwenye
makontena. Na endapo mizigo inayoletwa hadi kwenye forodha na kushushwa
kwa ajili ya kusafirishwa kwa magari ya mhusika ni lazima zoezi hilo
lifanyike eneo la forodha na kusimamiwa watendaji wa forodha”
Alifafanua Bw. Majaliwa.
Mhe. Dkt. Kijaji alipokuwa
akiongea na baadhi ya wasafirishaji wa mizigo, walimueleza changamoto
kubwa wanayokabiliana nayo ni kukaa siku mbili kwenye eneo la forodha
wakisubiri taratibu zikamilike ili waweze kuvusha mizigo yao.
Kwa upande wa forodha tatizo
kubwa lililopo ni miundombinu, “Eneo hili halina lani hivyo kupelekea
magari ya mizigo kupita kwa shida sana hasa kipindi cha mvua na
kusababisha magari kuharibika, hivyo ameiomba serikali iliangalie kwa
karibu ili kutatua kero hiyo” Alisema Bw. Majaliwa.
Kuhusu suala la vishoka Mhe. Dkt.
Kijaji aliwasisitiza Mamlaka ya Mapato hasa walioko kwenye forodha
kufanya jitihada za ziada kuhakikisha elimu ya mlipakodi inawafikia
walengwa na itolewe kwa ngazi zote. Na kuwataka watumishi wa Mamlaka
kuzingatia maadili katika utendaji kazi ili waweze kufikia lengo
lililokusudiwa.
Tags
HABARI KITAIFA