Wekundu wa Msimbazi Simba wameunguruma Mkoani Morogoro kwa kuitungua timu ya Burkina Faso kwa bao 3-0 kwenye mchezo wa Azam Sports Federation Cup (FA) mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Hamis Kiiza ametupia bao mbili kwenye mchezo wa leo, Kiiza alizama wavuni dakika ya 77 na kuipa Simba bao la kuongoza kabla ya kukwamisha tena bao lake la pili dakika ya 90 ambalo lilikuwa ni la tatu kwenye mchezo wa leo.
Goli jingine la Simba lilifungwa na Said Ndemla akiungana na Kiiza kuipa Simba ushindi kwenye mechi ya ugenini.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kusonga mbele kwenye hatua ya raundi ya nne ya mashindano hayo.
Matokeo ya mechi zote za leo michuano ya FA (Azam Sports Federation Cup) ni kama ifuatavyo:
(Jamhuri, Morogoro) Burkina Faso 0-3 Simba SC
(Nagwanda, Mtwara) Ndanda FC 5-0 Mshikamano
(CCM Kirumba, Mwanza) Pamba 1-4 Toto Africans
Ratiba ya michezo ya kesho:
(Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam) Yanga SC vs Friends Rangers
(Amaan, Njombe) Njombe Mji Vs Prisons
(CCM Kambarage, Shinyanga) Stand Untd Vs Mwadui FC
Tags
MICHEZO KITAIFA