Sasa ngoja tuangalie taarifa zilizopo kwenye headlines za vyombo vya habari vya Hispania.
3. Barcelona kumsaini mchezaji anayewaniwa na ArsenalInaripotiwa Barcelona wamepeleka offer yao ya mwisho kwa mchezaji ambaye amekuwa akiwaniwa na Arsenal kwa muda mrefu Nolito kutoka klabu ya Celta Vigo. Miamba hiyo ya Catalan inataka kumsajili striker huyo mwenye miaka 29 kwa mkopo lakini kukiwa na kipengele cha kumsajili jumla.
Rais wa Celta Vigo Miguel Torrecilla amemwambia Luis Enrique kulipa (£13.6m, $19.5m) ili kumnasa mchezaji huyo jumla kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.
Nalito amewahi kucheza kwenye kikosi cha Barcelona B kabla ya kujiunga na Celta Vigo na kwa mujibu wa wakala wake, kijana huyo anataka kurejea Camp Nou. Nalito amefunga magoli 8 kwenye mechi 10 alizocheza msimu huu.
2. Real Madrid yaanza mazungumzo na Neymar
Ripoti kutoka Hispania zinadai kwamba Real Madrid wamefungua mazungumzo na wakala wa Neymar kwa kile kinachodaiwa kuwa ni jitihada za kumhamishia star huyo kwenye dimba la Santiago Bernabeu.
Kwa mujibu wa mwandishi Eduardo Inda, Madrid watakuwa tayari kumlipa mshahara mara mbili nyota huyo (25-30m) juu ya euro 180 ambazo watatakiwa kulipa kumsaini..
Fiorentina Perez pia amemtaja kiungo mchezeshaji wa Chelsea Eden Hazard na golikipa wa Manchester United David De Gea. Neymar amefunga mabao 20 kwenye michezo 15 aliyoichezea Barcelona msimu huu.
1. Pique ashinda tuzo mbele ya Messi
Mlinzi wa kati wa Barcelona Gerrard Pique ametangazwa mchezaji bora wa Catalan wa mwaka 2015. Beki huyo wa zamani wa Manchester United amewapiku wapinzani wenzake akiwemo kiungo wa Barcelona Andreas Iniesta.
Amemshukuru kila mmoja kwa ajili ya tuzo hiyo kwa kusema: “Wamenipa kila kitu maishani. Nafahamu hizi tuzo ni muhimu sana kwao”.
Barcelona pia imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka, japo hilo lilikuwa ni jambo la kawaida na kila mtu alikuwa anatarajia hivyo kwa wakati huu
Tags
MICHEZO KIMATAIFA