………………………………………..
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesisitiza kauli yake kwamba tarehe iliyopangwa kati
yake na Mameneja wa Tanesco nchi nzima ya kuhakikisha inawaunganishinia umeme wateja waliolipa kwa kipindi kirefu ikiwemo kukamilisha matatizo ya LUKU bado iko palepale.
yake na Mameneja wa Tanesco nchi nzima ya kuhakikisha inawaunganishinia umeme wateja waliolipa kwa kipindi kirefu ikiwemo kukamilisha matatizo ya LUKU bado iko palepale.
Profesa Muhongo
ameyasema hayo leo wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas
Kandoro na kuongeza kuwa tarehe 15 Januari,2016, ndio tarehe ya mwisho
ya kukamilisha shughuli hizo nchi nzima.
“Katika hili nasema
kweli hakuna mzaha. Hatutanii. Wananchi wamechoka, wanataka umeme.
Mtindo wa kuandikiana barua tena haupo. Ukishindwa , unajiondoa
mwenyewe”,amesisitiza Prof. Muhongo.
Akijibu hoja za Kandoro
kuhusu suala la Makaa ya mawe, amesema atahakikisha suala hilo linapata
ufumbuzi wa haraka kuhakikisha rasilimali hiyo inatumika kama chanzo
kingine cha kuzalisha umeme nchini.
“Mkuu wa Mkoa hili
lazima tulishughulikie. Hatuwezi kuacha makaa ya mawe yakae tu kama
mapambo wakati tunahitaji sana nishati ya umeme kwa ajili ya kuondoa
matatizo ya umeme tuliyonayo”.
Prof. Muhongo ameongeza
kuwa, tayari amewaagiza wawekezaji wote wa makaa ya mawe wenye leseni
kukutana nae katika ziara ili kukubaliana kuhusu suala hilo.” Tayari
nimewaambia wote tukutane huku huku site wanieleze wanafanya nini”,
ameongeza.
Akieleza kuhusu suala la
matatizo ya maji katika vyanzo vya uzalishaji umeme, Prof. Muhongo
ameiagiza Tanesco Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, kuhakikisha wanaandaa
kikao cha wakuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Morogoro na Mbeya ili
kufanya tathmini ya utumiaji maji bila kuathiri pande zote ikiwemo
kutumika kwa ajili ya umeme na kilimo.
“Najua maji yanahitajika
sana katika kilimo hususan kilimo cha umwagiliaji ambacho ndio cha
kisasa. Lakini hata nishati inahitaji maji. Nawaomba kutaneni zungumzeni
halaf tembeleeni maeneo ya mabonde na mashamba mpate data zote,
mkimaliza tuangalie suala la kisera linasemaje . Suala hili ni muhimu
sana kwa ustawi na maendeleo ya uzalishaji nishati na kilimo. Lakini pia
tunahitaji kuwa na tamko la pamoja,” amesema Prof. Muhongo.
Aidha, Prof Muhongo
ameagiza kuwa katika kikao hicho kiwakutanishe pia na Wakuu wa mabonde
ili suala hilo liweze kujadiliwa na pande zote.
“Mkuu wa Mkoa nashauri
na wakuu wa mabonde wawepo. Lakini pia wanatakiwa kuangalia suala la
utoaji vibali kwa sababu kuna umwagiliaji mwingine sio mzuri”.
Wazalishaji wadogo wanalia sana na suala la uharibifu wa vyanzo vya
maji. Nimepita maeneo mengi wengi wanalia na wana hofu na maji. Wale
wanatusaidia sana kuongeza kiwango cha uzalishaji umeme. Kwetu sisi
wazalishaji wadogo ni muhimu sana”, amesema Waziri Muhongo.
Awali Mkuu wa Mkoa
alimweleza Prof. Muhongo kuhusu suala la Makaa ya mawe ya Kiwira na
kumweleza umuhimu wa kuendeleza miradi hiyo kwa maendeleo ya nchi na
katika kusaidia taifa kuwa na kiasi cha umeme wa kutosha.
” Prof. nashauri sana
wizara yako ifufue mgodi wa Kiwira kutokana na umuhimu wake kwa taifa.”
Awali mgodi huu ulikuwa unasaidia kuingiza umeme kwenye gridi hii ni
muhimu. Mkoa wetu umebarikiwa kuwa na madini na ni wa tatu katika
kuchangia pato la Taifa. Tukiongeza na Kiwira taifa litanufaika zaidi,”
ameongeza Kandoro.
Akiwa mkoani Mbeya Prof.
Muhongo atatembelea mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira, Wachimbaji wadogo wa
madini Chunya, maeneo yenye viashiria vya nishati ya jotoardhi Mbaka,
Bonde la mto Songwe kwenye mradi wa kuzalisha umeme na maeneo mengine.
Tags
HABARI KITAIFA