WAZIRI wa nchi
ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI)George
Simbachawene amemvua cheo ha Ukurugenzi Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Agustino
Kalinga kwa kushindwa kuwasimia watumishi waliopo chini yake.
Pia Waziri
huyo amemsimamisha kazi Ofisa elimu
vifaa na takwimu msingi wa manispaa hiyo Josephine Akimu kwa kosa la
kudharau maelekezo ya kiongozi wake kwa kusaini barua kwa niaba ya Mkurugenzi
huku akitumia jina la Afisa elimu wake bila ridhaa yake.
Hatua hiyo
ilitangazwa jana mjini hapa na Waziri Simbachawene wakati alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari.
Waziri huyo
alisema kuwa kutokana na kubainika kwa kasoro katika Shule ya msingi Dodoma
Makulu ya kuandikwa kwa barua toka ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ikielekeza
uchangishwaji fedha kwa wazazi wa michango ya maji,umeme na mlinzi michango
ambayo ilishafutwa na Serikali.
“Mkurugenzi
huyu wa Manispaa ya Dodoma Kalinga ameshindwa kuwasimamia watumishi walio chini yake hadi
kusababisha kuandikwa na kusambazwa barua kwa walimu wakuu wa shule za msingi
Manispaa ya Dodoma ambayo inatofautiana na maelekezo ya serikali yaliyopo
kwenye mwongozo,”alisema
Pia
alisisitiza kuwa Mkurugenzi huyo
ameshindwa kusimamia utekelezaji wa maelekezo sahihi ya serikali kuhusu
utoaji wa elimu msingi bila malipo hivyo
namvua cheo hicho ili hatua nyingine ziweze kuchukuliwa .
Aidha Waziri
huyo amempa onyo Ofisa wa elimu msingi
wa Manispaa ya Dodoma Scola Kapinga kwa
kosa la kutokuwa makini na idara yake hadi kusababisha barua hiyo kuandikwa na
kupelekwa shuleni bila yeye kuwa na taarifa.
“Nawaagiza
wakuu wa mikoa,m wa mikoa,wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mamlaka za Serikali
za mitaa kuendelea kuwaelimisha wakuu wa shule za msingi na sekondari katika
maeneo yao kuhusu utoaji wa elimu bure bila malipo.
Wiki iliyopita Waziri George Simbachawene akiambatana na Naibu
katibu mkuu Tamisemi elimu,Bernard Makali alifanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya msingi Dodoma Makulu kujionea hali
halisi ya mgawanyo wa fedha za elimu bure na kubaini barua toka Ofisi ya
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma iliyoandikwa na Ofisa elimu msingi kuelekeza michango ya fedha za maji,umeme na mlinzi kwa wazazi.
Tags
ELIMU