Afisa
Uhamiaji Mkoa wa Mbeya Ndugu Asumsyo Achacha akizungumza ofisni kwekwe
juu ya zoezi linaloendelea la kuwasaka wahamiaji haramu mkoani humo.
Na jamiimojablogu,Mbeya
Zoezi
la kuwasaka wahamiaji haramu na wageni wanaofanya kazi bila kibali
limeendelea kufanikiwa mkoani Mbeya ambapo jumla ya wageni 20
wamekamatwa mkoani humo kutokana na makosa mbalimbali likiwemo la
kuingia nchini kinyume cha sheria.
Akizungumza na waandishi wa
habari Ofisini kwakwe Afisa uhamiaji Mkoa wa mbeya Ndugu Asumsyo Achacha
amesema hatua hiyo imefanyika ikiwa ni kutekeleza majukumu yao ya kila
siku sanjali na kutekeleza agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Charles
Kitwanga alilotoa hivi karibuni.
Aidha amesema hatua hiyo ni
utekelezaji wa sheria mpya ya kuratibu ajira za wageni ,Sherii Na.1 ya
mwaka 2015 ambayo inawataka wageni wote walioajiliwa hapa nchini kuwa na
vibali vya kazi na hati za ukaazi nchini.
Afisa uhamiaji huyo
amewataja raia hao waliokamatwa katika msako huo ni pamoja wakenya
watatu (3)wamalawi 14 pamoja na wakongo watatu (3).
Aidha amesema
kuwa mwaka 2015 jumla ya wahamiaji haramu 478 kutoka mataifa mbalimbali
walikamatwa na kuchukuliwa hatua mbalimbali ikiwemo kufikishwa
mahakamani pamoja na kufukuzwa nchini.
Amesema mbali na
changamoto zilizojitokeza ikiwemo upungufu wa vitendea kazi ,fedha
pamoja na rasilimali bado shughuli za uhamiaji mkoani humo ziliendelea
kufanyika kama kawaida na kwa ufanisi mkubwa.
Pia Afisa Uhamiaji
huyo amebainisha kuwa zoezi hilo ni endelevu hivyo ofisi yake
itahakikisha kila mtu aliyevunja sheria anakamatwa hivyo ametoa wito kwa
waajiri kuacha tabia ya kuwapa ajira wafanyakazi wa kigeni wasio na
vibali vya kazi na ukaazi kwani msako huo utaendelea katika viwanda
,migodi mashuleni na mahotelini.
Mwisho. |