…………………………………………………………..
Na Nyakongo Manyama
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wanatarajia
kutoa elimu, huduma na vipimo vya bure vya magonjwa ya saratani ili kuiwezesha jamii
kujikinga na ugonjwa huo nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo (Jumatano) Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Dkt. Ulisubisya Mpoki huduma hizo za matibabu na vipimo
vitaenda sambamba na maadhimisho ya siku ya saratani
duniani inayoathimishwa ulimwenguni kote tarehe 4. Februari ya kila mwaka.
Aidha Dkt. Mpoki aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili wapate huduma ya kupima ugonjwa wa saratani katika
katika Hospitali ya Ocean Road ili kujihadhari na maambukizi ya ugonjwa huo.
“Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road tunapenda
kuwaambia wananchi wote wajitokeze kupima ugonjwa huo ikiwemo saratani ya tezi
dume kwa wanaume na saratani ya matiti kwa wanawake bila ya malipo” aliongeza
Dkt. Mpoki.
Dkt. Mpoki amewataka watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata vipimo na matibabu ya
saratani ya ngozi na kuwataka wajilinde ili wasipate miale ya jua inayoathiri
ngozi zao na kupelekea maambukizi ya ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa Dkt. Mpoki alisema ugonjwa wa saratani huchangiwa zaidi na ulaji usiozingatia kanuni za afya,matumizi
ya vilevi, uvutaji wa sigara na matumizi ya makubwa ya sukari.
Kaulimbiu ya Maadhimisho yaSiku ya Saratani Duniani mwaka huu ni ‘TUNAWEZA, NINAWEZA. KWA PAMOJA TUWAJIBIKE KUPUNGUZA
JANGA LA SARATANI DUNIANI.”