Kutoka
kulia ni Msanii Mrisho Mpoto, Abdallah Mkumbila (Muhogo Mchungu),
Mudhihir Mudhihir, Majid Mswahili Majidi na Masoud Kipanya wakizindua
kitabu cha Mwele bin Taabani.
Mudhihir Mudhihir ambaye ndio mtunzi wa kitabu hicho akielezea maudhui ya kitabu kwa ufasaha.
Majid
Mswahili, mchambuzi wa maswala ya kiuchumi,siasa na jamii kutoka katika
Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo.
Abdallah
Mkumbila (Muhogo Mchungu) akielezea baadhi ya vipengele vya kitabu huku
akiwasihi watanzania kukisoma kitabu hicho kwani kina mafunzo kwa
wanajamii.
…………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
Mudhihiri Mohamed Mudhihiri ambaye
ni mwanasiasa mkongwe na mtunzi mahiri wa vitabu leo hii jijini Dar Es
Salaam amezindua kitabu chake cha Riwaya ya Mwele Bin Taaban.
Kitabu cha Mwele bin Taabani, tayari ameshakiingiza sokoni, kimebeba uhalisia wa maisha ya Mtanzania wa hali ya chini ambaye anakumbana na madhila, ambayo msingi wake ni utawala na watawala wanaojali zaidi masilahi yao, kuliko ya wapiga kura wao.
‘Mwele bin Taabani’ ni riwaya inayoyaakisi magumu ya Watanzania wengi hasa wa vijijini ambao wanalima sana, lakini wanavuna kidogo huku wakikosa watu wa kuwasemea na kusikiliza matatizo yao pamoja na kuwapo kwa Serikali ambayo imekuwa ikikusanya kodi kila uchwao kwenye mazao yanayozalishwa na mafukara hao.
Ukifanikiwa kukisoma kitabu hicho na kukielewa, hakika utakubaliana na mtunzi wake kuwa amedhamiria kufikisha sononeko la wananchi masikini kwa viongozi Serikalini.
Kwa kulifahamu hilo, Mudhihiri kwa kauli yake amesema kitabu hicho kinafaa sana ndani ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwani ndiyo mkongojo mujarabu kwa masaibu ya Wanakazamoyo (Wananchi).
Mbali na kitabu cha Mwele bin Taabani, vingine vipo kwenye ngazi ya muswaada ambavyo ni Msaliti, Nyungu ya Mawe, Nasaha za Mswahili na Viungo vya Ushairi.
Kwa mujibu wa Mudhihiri, tafsiri ya Mwele ni mgonjwa. Mwele bin Taabani kwa muktadha wa riwaya hii si mwanadamu bali ni kadhia ya ustawi duni wa jamii ya Wanakazamoyo.
Pia kitabu hiki kinafaa mashuleni na vyuoni. EMAC wametaka kitumike kidato cha tano na sita na vyuoni pia na hivi sasa Wahadhiri nchini wameonesha dhamira ya kukitumia kitabu hiki katika fasihi kwa ngazi ya uzamili.
Mikakati inaendelea ili kukifikisha kwenye maeneo mbalimbali ya nchi kwa bei nafuu isiyozidi shilingi 6,500.

Tags
KIBURUDANI