Na.Catherine Sungura-Nzega
Serikali haitokuwa tayari kuwaona
watumishi wa umma wachache wakinufaika na kufaidi pesa za walipa kodi
hususan wa kipatao cha chini na wale maskinini
Hayo yamesema wilayani hapa na
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,
Dkt.Hamisi Kigwangwalla alipokuwa akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo
Dkt.Kigwangwalla alisema serikali
ya awamu ya tano inawataka watumishi wote nchini kufanya kazi za
kuwahudumia wananchi na kuacha uzembe kwani awamu hii haiwezi
kuwavumilia watumishi wa namna hiyo.
“Serikali haitowav umilia
watumishi wazembe,hivyo tutaendelea kuwafungia mageti na kuwashughulikia
wale wazembe,tunataka watumishi wa umma wafanye kazi ya kuwahudumia
wananchi kwa ufanisi,mtumishi akizembea tutamtumbua majipu,akichelewa
tunamfungia geti na akiiba tunafilisi pamoja na kumpeleka jela,hii ndiyo
serikali ya hapa kazi tu”
Aidha alisema serikali ya awamu
ya tano inataka kero za wananchi zifanyiwe kazi na kutekeleza ahadi zote
za ilani ya uchaguzi ya ccm zinatimizwa.
“hatutomuonea mtu,lakini
tutafanyia kazi pale penye matatizo,tunataka Tanzania mpya ya mwaka 2015
inakua,hatutaki hadithi wala ahadi”
Hatahivyo aliwataka wazazi wote
wenye watoto wenye umri wa kwenda shule kuwapeleka watoto wao kuanza
masomo kwani elimu kwa sasa ni bure na hakuna michango yoyote.
“natoa wito kwa walimu wote
wasitoze michango yeyote wala ushuru kwa wazazi wanaowapeleka
kuwaandikisha watoto shule kwani shule zimepatiwa pesa za kuendeshea
shule hizo.
Dkt. Kigwangwalla aliwakumbusha
watumishi wa umma kujipanga na kama watagundulika ni majipu bali
hawatosita kuwatumbua hadi kina kitoke,usaha na damu kutoka bila huruma
Tags
AFYA