Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Suleiman Jafo akijibu maswali toka
kwa wabunge katika kikao cha 6 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini
Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
………………………………………………………………………………………………….
(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
Serikali katika mwaka wa fedha
2016/2017 imepanga kuongeza ajira kwa vijana ili kukabiliana na
changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania kwa
kuongeza ajira na kuwezesha wengine kujiajiri kupitia mifuko ya
uwezeshaji toka Halmashauri za Wilaya nchini.
Akijibu swali la Mhe.Mgumba
Tebweta Omary Mbunge wa Morogoro Kusini (CCM) lenye sehemu a na b
lililouliza Serikali itaanza lini kuwawezesha vijana wa Jimbo la
Morogoro Kusini Mashariki kifedha ili waweze kujiajiri na kuondokana na
tatizo la ajira na umaskini ,Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe Suleiman Jafo amesema vijana
katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Kusini Mashariki wamekuwa
wakiwezeshwa kiuchumi kupitia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
ambapo kila Halmashauri hupaswa kutenga asilimia 5 ya mapato yake ya
ndani kila mwaka kwa ajili ya vijana.
Mhe Suleiman Jafo ameongeza kuwa
katika Bajeti ya mwaka 2014/2015,Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro
ilifanikiwa kutoa Shillingi Millioni 10.3 kwa vikundi vya vijana 19 kwa
ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi na katika Bajeti ya
mwaka wa fedha 2015/2016 vikundi vya vijana vilitengewa Shilllingi
Millioni 87.5 ili kuviwezesha kiuchumi kwa kujiajiri.
“ Katika kutatua changamoto
zilizopo kwa vijana tunawawezesha kifedha ili kujiajiri ili kumekuwa na
tatizo la fedha kuchelewa kufika kwa walengwa ila Serikali kupitia
Wizara yangu tunalifanyia kazi ili fedha zifike kwa wakati na tumetenga
Shillingi Millioni 50 kwa kila kijijikwa ajili ya kuwezesha vijana
walioko katika vikundi mbalimbali mfano SACCOS ili waweze kujiajiri na
kujikwamua kiuchumi kwa kujiondoa katika hali ya umaskini”
“ Napenda kuwaomba wabunge
tusaidiane sababu wao wanahusika katika kamati za fedha za Halmashauri
za Wilaya, waende wakasimamie hizo fedha kwa ajili ya kuwezesha vijana
zitoke na ziwasaidie walengwa” Alisema Mhe Jafo.
Aidha Mhe Suleiman Jafo amesema
kuwa Serikali imetenga Shillingi Billioni 233 kwa ajiri ya kuajiri
vijana wapya takribani 71,408 kati ya hao watumishi wapya wa Afya
wanatarajiwa kuwa takribani 10,871 na Waalimu 40,000 kwa nchi nzima ili
kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo mbalimbali nchini.
Serikali kupitia Halmashauri za
Wilaya imejipanga katika kuwawezesha vijana katika maeneo yao kujikwamua
kiuchumi kwa kujiajiri na kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali
itaboresha zaidi mifuko ya kuwezesha vijana katika Halmashauri za Wilaya
kwa kununua vifaa zaidi vya kujifunza stadi mbalimbali za kazi
zitakazowezesha vijana wengi zaidi kuwa na ujuzi utakaowasaidia
kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi.
Tags
HABARI KITAIFA