Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
akisimamia maandalizi ya wodi mpya ya wazazi katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili jana. Rais John Magufuli aliamuru jengo lililokuwa likitumiwa
kwa huduma za Uzazi na Mtoto kutumiwa kama wodi ya wazazi kuanzia leo.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
akisimamia maandalizi ya wodi mpya ya wazazi katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili jana. Rais John Magufuli aliamuru jengo lililokuwa likitumiwa
kwa huduma za Uzazi na Mtoto kutumiwa kama wodi ya wazazi kuanzia leo.
……………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Waziri wa Afya ,maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu amewasimamisha
wakurugenzi toka Bohari ya Dawa ya Taifa(MSD) kwa ubadhilifu wa fedha
takribani Shillingi Billion 1.5.
Ameyasema hayo wakati akizungumza
na Waandishi wa Habari katika Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto baada
ya kupokea vifaa toka Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa (MSD) amesema amepata
taarifa ya uchunguzi ofisini kwake ya ubadhilifu wa kiasi hicho cha
fedha na kuamua kuwasimamisha wakurugenzi wanne kupisha uchunguzi.
“ Nimepata taarifa toka ofisini
kwangu na nimeamua kuchukua fursa hii kuwaambia na hili pia kwamba
nimewasimamisha wakurugenzi wanne toka Bohari ya Kuu Dawa ya
Taifa,nisingeweza kusubiri nitumbuliwe mimi jipu na Mhe.Rais kwahiyo
nimeamua kuwachukulia hatua kwa kuwasimamisha kazi ili kupisha
uchunguzi”
“ Hizi ni zama za kufanya kazi na
kuwajibika sasa inabidi tuwajibike kwa kufanya kazi na hatutowavumilia
watendaji watakaoenda kinyume na utaratibu katika ofisi yoyote ile
katika sekta ya afya na tutawachukulia hatua kwani tunataka uwajibikaji
ili kuiendeleza sekta ya afya ambayo ni muhimu sana kwa kila mwanadamu”
Alisema Ummy.
Amewataja aliowasimamisha kazi
kuwa ni Joseph Tesha Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Misanga Muja
Mkurugenzi wa Ugavi, Heri Mchunga Mkurugenzi wa Manunuzi na Cosmas
Mwaifani Mkurugenzi Kanda na Huduma kwa Wateja ambapo amewataka
Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya Dawa ya Taifa kuwaandikia
barua mara moja ya kuwasimamisha kazi.
Katika kuboresha sekta ya afya
nchini Wizara wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee
imejipanga kufanya kazi kwa taratibu na misingi iliyopo ili kuhakikisha
inapeleka mbele gurudumu la maendeleo ya hasa katika sekta ya afya kwa
ujumla.
Tags
AFYA