BANDA MEDIA BLOG

Ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano


ba1
Naibu Waziri wa  Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (katikati) akielekezwa jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo  Bw.Magid Hemed  alipofanya ziara yake ya kutembelea Wilaya hiyo kwa kuangalia mradi wa ujenzi wa daraja la Ruvu chini na bandari ya Bagamoyo.
ba2
Naibu Waziri wa  Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (katikati) akionyeshwa ramani itakapojengwa bandari ya Bagamoyo kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa Upanuzi wa Bandari hiyo kutoka Mamlaka  ya Bandari nchini  Bw. Alexender  Ndibalema (Kushoto)  katika ziara yake ya   kutembelea Wilaya  ya Bagamoyo .
ba3
Eneo ya Chuo cha Uvuvi  cha Mbegani Wilayani Bagamoyo  ambayo ipo katika mpango wa kubadilishwa na kuwa Bandari ya Bagamoyo .

ba4
Naibu Waziri wa  Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kulia) akisalimiana na Mafundi  wa  kampuni ya Ujenzi ya ESTIM inayojenga daraja la Ruvu chini katika barabara ya Bagamoyo kwenda Msata   katika ziara yake ya   kutembelea Wilaya  ya Bagamoyo .
ba5
Naibu Waziri wa  Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kulia) akielekeza jambo wakati alipotembelea ujenzi wa daraja la Ruvu chini  katika barabara ya Bagamoyo kwenda Msata , wanaongalia  ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Magid Hemed (katikati) na Kushoto ni Mbunge wa Bagamoyo Mhe. Shukuru kawambwa
ba6
Naibu Waziri wa  Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kushoto) akimsikiliza  Mhandisi wa mradi wa ujenzi wa daraja la Ruvu chini Bw. Adam Makiba(Kulia) wakati wa ziara ya kutembelea Wilaya ya bagamoyo pamoja na miradi ya ujenzi wa Bandari na daraja .
ba7
Ujenzi wa daraja la Ruvu chini unavyoonekana katika picha  ambapo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.
ba8
ba9
Naibu Waziri wa  Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kushoto) akipata maelezo kuhusu ukarabati wa barabara ya Msata kutoka kwa   Mhandisi wa mradi wa ujenzi  huo  Bw. Adam Makiba wakati wa ziara ya kutembelea Wilaya ya bagamoyo pamoja na miradi ya ujenzi wa Bandari na daraja la Ruvu chini .

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG