MTU mmoja mwenye umri wa miaka 80
amekutwa akiwa amefariki ndani ya choo cha msikiti wa Ibadhi ulioko
Bopwe karibu na Ofisi za Baraza la Wawakilishi Wilaya ya Wete Mkoa wa
Kaskazini Pemba .
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi ofisini Kwake , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba
Kamishina msaidizi Hassan Nassir Ali alisema aliyefikwa na mauti hayo
kuwa ni Hassan Ali Juma mkaazi wa Bopwe Wete .
Alisema mzee huyo aliondoka
nyumbane kwake machi 9majira ya saa saba , kuelekea msikitini kwa ajili
ya maandalizi ya swala ya adhuhuri , na kuonekana machi 10 majira ya
saa 12.45 jioni akiwa amefariki ndani ya choo .
Inadaiwa kuwa mzee huyo baada
ya kufika msikitini aliingia chooni kisha kufunga mlango kwa ndani
ambapo alianguka akiwa katika harakati za kufua fulana alilokuwa amevaa
ili aoge.
“Tumebaini kwamba mzee huyo
alianguka katika harakati za kuvua fulana , ambapo tumemkuta akiwa
amefunikwa na fulana usoni huku akionekana kuumia zaidi sehemu za
kichwani ”alifahamisha .
Akizungumza katika eneo la tukio
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jina wa jeshi la Polisi Mkoa hu . Issa
Juma Suleiman aliwataka wananchi kutoa taarifa katika jeshi la Polisi
wanapopotelewa na jamaa zao ili wasaidiane kuwatafuta .
Alieleza kwamba tangu mzee huyo
alipopotea hakuna mtu aliyefika na kutoa taarifa katika jeshi la Polisi
jambo ambalo ni kinyume na utaratibu .
Naye mdogo wa marehemu Khamis Ali
Juma (42) alisema kabla ya kufikwa na mauti hayo kaka yake hakuwa na
matatizo yoyote kiafya , na aliondoka nyumbani kwa ajili ya kuwahi swala
ya Adhuhuri katika mskiti wa Ibadhi .
Mashuhuda wa tukio hilo
walifahamisha baada ya kuona mlango umefungwa walichungulia na kumuoa
akiwa amelala chini , ndipo juhudi za kuvunja zilichukuliwa chini ya
usimamizi wa jeshi la Polisi .
Ali Salim Chande aliiambia gazeti
hili kuwa mlango ulipovunjwa walimkuta akiwa ameumia sehemu za
kichogoni na tayari harufu mbaya alikuwa imeanza kutoa kutokana na
kutokwa damu .
Kifo cha Mzee Hassan kimeacha
pengo kwa wajasiriamali kwani alikuwa mstari wa mbele kuwashawishi
vijana kujiajiri wenyewe na kuacha kutegemea ajira za Serikali .
Mzee Hassan ambaye alikuwa
mjasiriamali aliywa kuwa akiuuza vyngu vya udongo alizikwa jana katika
makubiri yaliyoko Piki sehemu aliokozaliwa .
Tags
HABARI KITAIFA