…………………………..
Hospitali ya Kairuki (KH) inatimiza miaka 29 mwezi huu siku ya Alhamisi tangu ilipoanzishwa tarehe 17.03.1987.
Akizungumzia maadhimisho hayo Dr
Asser Mchomvu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki anasema
kuwa uongozi wa KH unapenda kuwashukuru wadau wote walioshirikiana nao
katika kuiwezesha KH kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa wote.
Dr Mchomvu anaongeza kuwa katika
kutambua mchango wa wadau mbalimbali kwa kufikisha miaka 29, KH itafanya
maadhimisho yake kwa kutoa msaada kwa vituo vya afya pia kufanya
upimaji wa kinywa na meno bure.
“Madhimisho haya yataambatana na utoaji wa vifaa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha, ambapo KH itatoa msaada wa vitanda vya hospitali na magodoro siku ya Alhamis tarehe 17.03.2016,” alisema Dr Mchomvu
Alisisitiza kuwa pamoja na hilo, KH itatoa pia huduma ya upimaji na ushauri wa afya ya kinywa na meno kwa wananchi kwa siku mbili bure ( siku ya Jumatano na Alhamis tarehe 16 na 17, Machi 2016) kuanzia saa 2 asubuhi, pale pale Hospitali ya KAIRUKI, Mikocheni, Dar es Salaam.

Dr Mchomvu anaeleza kuwa,
kutakuwa na ghafla fupi ambapo Mkurugenzi atatoa salamu baada ya kukata
keki na watoto waliozaliwa KH mwaka 1987. Watu wote wanakaribishwa
katika ghafla hiyo itakayofanyika hapo KH siku hiyo ya Alhamisi tarehe
17.03.2016 saa 10 jioni.
Kwa upande mwingine KH imekuwa
mstari wa mbele katika kutoa huduma zake huku ikizingatia ufanisi na
ubora katika utowaji wa huduma zake kwani inatumia vifaa vya kisasa
ambavyo vina ubora wa hali ya juu.
Tags
AFYA