Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipiga ngoma alipokuwa akiwasili katika
ukumbi wa Golden Jubelee Towers alipokuja kushiriki katika uzinduzi wa
Video mpya ya Mshairi Mrisho Mpoto inayoitwa Sizonje .Wengine Pichani ni
Mrisho Mpoto,Dr Mwaka na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi leah
Kihimbi.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye Nape Nnauye akizindua rasmi video ya
Sizonje,Kushoto kwake ni Mrisho Mpoto.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiinadi video ya Sizonje kwa wadau
mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi huo.Nape aisema video hiyo
inawakilisha serikali ya awamu ya tano na utumbuaji wa majipu.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Msichana
Butogwa Charles Shija aliyeongoza kitaifa katika mtihani wa kidato cha
nne.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Congcong
Wang aliyeshika nafasi ya pili kitaifa katika mtihani wakidato cha nne.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha ushujaa kwa kijana
Salmin Selemani ambae alifanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne
lakini hakukata tamaa na kujitokeza hadharani ili asaidiwe,Waziri Nape
amejitolea kumwendeleza kijana uyu.Picha na Daudi Manongi.
…………………………………………………………………………………………………………
Na Daudi Manongi-WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye amewataka watanzania kutumia utamaduni wetu kujenga nchi yetu.
Waziri nape ameyasema hayo wakati
wa uzinduzi wa video ya mshairi Mrisho Mpoto mbele ya wadau mbalimbali
wa sanaa kutoka kila kona ya jiji la Dar es Salaam waliofurika kuangalia
uzinduzi huo ulioendana sambamba na mada kubwa mbili za utamaduni na
lugha na kauli mbiu ya Kufeli elimu sio mwisho wa maisha.
“Serikali ya awamu ya Tano
imejipanga vyema katika kutumia utamaduni wa nchi yetu kushape vijana
wetu wawe na morali,wajitambue ili wafike mbali,tutatumia utamaduni huu
kujenga nchi yetu kikamilifu kwani ni silaha tosha kuvutia hata nchi
nyingine.Maisha sio rahisi,ni kuvumilia,kutokata tamaa na kuweka
malengo.Safari tumeianza na tutafika mbali”Alisema Nape.
Pia Waziri uyo aliwataka
watanzania kumuunga mkono Mrisho mpoto na kutomkatisha tamaa kwani
anamsaidia rais wa awamu ya Tano Mhe.John Pombe Magufuli katika kutumbua
majipu.Mbali na hilo alimshauri Mrisho mpoto kwenda mikoani kwani hata
uko kina Sizonje wapo wengi muwaonyeshe kwamba iko njia kwa watu
waliokata tamaa.
Kwa upande wake Mrisho mpoto
aliwasii watanzania kujenga taifa letu na pia tujenge Kiswahili na
kukitumia kama ajira kwani ni lugha ya sita kwa sasa duniani.
“Lazima tujue kwamba Kiswahili ni
lugha ya kibiashara,tuangalie fursa zilizopo kupitia Kiswahili
kujipatia ajira kwani nchi kama Namibia,Zimbabwe wamepokea Kiswahili na
wanaitaji kufundishwa zaidi na kwa namna hii izi zote ni fursa kwani
lugha imekuwa bidhaa sasa”Alisema Mpoto.
Wakichangia katika mjadala
uliopewa jina “kufeli elimu sio kufeli maisha” Bw.Ruge Mutahaba alisema
kufeli darasani kusikuzwe na kuwataka vijana kutengeneza maono mapema
kwani yatakuwa ndio mwongozo wa maisha yao yote na yatawafanya vijana
kutokata tama mapema.
“Vijana Mjifunze kuwasiliana,muwe
wabunifu,mjifunze kuwa na utaratibu wa kujifunza kitu kipya kila
siku,pia mtengeneze jamii ya watu ambao ni watatua matatizo na sio
watumikaji tu kwani kwenye matatizo ndo kwenye fursa zote,msiiachie
serikali pekee kushughulikia huduma za jamii bali tumieni mwanya huo
kuanzisha za kwenu”Alisema Ruge.
Naye mwakilishi kutoka TBL Bw
George Kavishe aliwataka vijana kujua mihimili yao pamoja na uwezo wao
na kwa kufanya ivyo watakuwa wamejua wapi wanacho na nini kinafaa
kufanya ili kuboresha maisha yao.
Mjadala huo pamoja na uzinduzi wa
video ya sizonje uliambatana na waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
michezo Mhe.Nape kuwapa vyeti vya pongezi na ushujaa vilivyoandaliwa na
Mrisho Mpoto wanafunzi waliofanya vizuri na wale waliofanya vibaya
katika mtihani wa kidato cha nne.
Tags
UTAMADUNI