Akizungumza na mbeyacityfc.com
mapema leo asubuhi kocha msaidizi wa City, Mohamed Kijuso amesema
kikosi kimewasili salama na leo watafanya mazoezi ya jioni kwenye
uwanja wa chuo cha Jordan kilichopo mkoani hapa yatakayofatiwaa na
program maalumu ambazo zitakuwaa zikiongozwa na Mwalimu Kinnah Phiri
kabla ya kuivaa Simba Siku ya jumapili jijini Dar.
“Tutakuwa uwanjani jumapili
dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Taifa,hilo ndiyo jambo kubwa naweza
kusema, tumesafiri na kufika hapa Morogoro hali za wachezaji wote 18
zikiwa salama, kwa hilo tunamshukuru Mungu,jioni ya leo tutafanya
mazoezi hapo chuoni Jordan na kesho tutakuwa na program maalumu amabazo
mwalimu ameziandaa” alisema.
Kuhusu Simba, Kocha huyo kijana
ameweka wazi kuwa timu hiyo kutoka mtaa wa msimbazi ni nzuri hivyo
hawataibeza hata kidogo licha ya matatizo kadhaa yaliyopo kwenye kambi
yake kwa sasa, na kusema kikosi chake kitaingia uwanjani kupambana kwa
nguvu zote kuhakikisha City inaibuka na ushindi.
“Nafahamu Simba wana matatizo
madogo kwenye kambi yao hivi sasa,jambo hilo halitufanyi kuwabeza, bado
ni timu nzuri na iko kwenye nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi
tofauti na sisi, tutaingia uwanjani kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha
tunaibuka na ushindi ili tuweze kujiimarisha zaidi, hivi sasa
tunahitaji matokeo kwenye kila mchezo jambo ambalo pekee litatutoa
tulipo na kutupeleka sehemu nyingine alisema”.
Akiendelea zaidi Kijuso alisema
kuwa, anafahamu Simba ina wachezaji wengi vijana na wenye kasi pia
inatumia nguvu nyingi kumiliki mpira kwenye eneo la kiungo hivyo ni
wazi City itatumia kikosi tofauti na kile kilichozoeleka huku mbinu za
kuhakikisha wanaziba nafasi zote kwenye eneo la katikati ya uwanja
zikiwa tayari zimeshafanyia kazi.
Tags
MICHEZO KITAIFA