Na. Lydia Kishia na John Banda
JESHI la polisi
Mkoani Dodoma limefanikiwa kukamata silaha 26 aina ya Gobole na mtambo
ya kuyatengezea kinyume cha sheria ya umiliki wa siraha.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa
habari kuwa Magobore 19 yamesalimishwa na wamiliki waliokuwa
wakiyamiliki kinyume na sheria baada ya kusikia wito wa Jeshi hilo
lililowataka kuzisalimisha.
Mambosasa
amesema jeshi hilo pia linawashikilia watu 7 wakazi wa Manda Wilayani
Chamwino baada ya kuwakamata na aina hiyo ya silaha 7 pamoja nyundo 1
risasi zilizotengenezwa kienyeji ambazo zinadaiwa zilikuwazikitumiwa
kuwindia wanyama katika poli la Ruaha mkoani iringa
Aidha
kamanda huyo amesema moja ya Gobole lilikuwa limevishwa shanga ambayo
ni ishara ya nguvu za Giza ili polisi wasifanikiwe kuikamata ambapo
pamoja na hilo wamefanikiwa kukamata pikipiki zenye makosa mbalimba 250
na kuwatoza wamiliki wake jumla ya million 7 na Laki 2 na 30 Elfu
Tags
HABARI KITAIFA

