SERIKALI imeanzisha mfumo wa
Kielektroniki wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao
unalenga kuondoa tatizo la madai ya malimbikizo ya stahili zao.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa jana (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na
watumishi wa sekta mbalimbali katika wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu alisema mfumo huo ujulikanao kama LAWSON, unatumika kwenye ajira za watumishi wote nchini, wa Serikali Kuu na wale wa Serikali za Mitaa
Waziri Mkuu alisema mfumo huo unasaidia kutunza, kutuma na kuhuisha taarifa za watumishi kwa wakati na kwa ufanisi tangu mtu anapoajiriwa hadi inapofikia wakati wa kupandishwa madaraja na hadi anapostaafu.

Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo
huo, maafisa utumishi walipaswa kukusanya taarifa za watumishi wote
walioajiriwa na kuzipeleka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
ili zikathibitishwe kabla ya kuzipeleka HAZINA kwa maandalizi ya
mishahara.
Akitolea mfano wa kada ya ualimu,
Waziri Mkuu alisema ajira za walimu zilikuwa zinaanzia Idara ya
Utumishi wa Walimu (TSD) lakini anapaswa aende kuripoti kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri (DED) ambaye ni mwajiri wake chini ya
TAMISEMI. “Hii ilileta ugumu wa malipo ya kupanda madaraja, uhamisho ama
likizo kwa sababu mwajiri anakuwa hajatenga hizo fedha.”
“Sasa hivi tuna Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) ambayo iko chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. Kwa hiyo ni rahisi wao kukaa pamoja na kuamua tuwapandishe daraja walimu 10 na wote hao wakalipwa bula bila kuchelewa,” alisema.

Alisema mfumo huo umeanza
kutumika tangu mwaka 2012 na ulianza kwa ajira mpya za wakimu na hadi
sasa umethibitisha kuwa inawezekana kumlipa mtumishi mshahara wake hata
kama ameajiriwa ndani ya mwezi huohuo.
“Kama mtumishi anaripoti kwenye
kituo kipya hata iwe wilaya ya wapi ili mradi amefika na barua zake zote
na ziko sahihi mtu huyu ataingiziwa taarifa zake na wakati huohuo
taarifa zitaonekanaOfisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na pia
zitapokelewa kwa maafisa wanaoshughikia mishahara kule HAZINA.”
Alisema changamoto pekee
waliyokutana nayo wakati mfumo huo umeanza ilikuwa ni kutoingizwa
taarifa za wale ambao wameripoti baada ya tarehe 10 ya mwezi husika.
“Hii ni kwa sababu matayarisho ya mishahara yanakuwa yameshaanza. Kwa
hiyo wengi walishauriwa kuripoti kati ya tarehe 25 hadi tarehe 9 ya
mwezi uliofuata na wote hawa hawakupata matatizo ya kucheleweshewa
mshahara,” alisema.
Akifafanua kuhusu upandishaji
madaraja ya watumishi, Waziri Mkuu alisema Serikali imeondoa utaratibu
wa mtumishi kulazimika kuandika barua ya kukiri kupandishwa daraja/cheo
ndipo aanze kupata stahili zake mpya. “Hii imeondoa ucheleweshaji wa
kufanyika marekebisho ya mshahara na pili imeondoa tofauti za mishahara
kwa watumishi wenye ngazi moja (sifa sawa za kitaaluma, tarehe moja ya
kuajiriwa) ambao walikuwa wakilipwa tofauti kwa sababu mmoja aliwahi
kuandika barua ya kukiri na mwingine alichelewa kuandika barua hiyo hiyo
” alisema.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa amelazimika kukatisha ziara ya mkoa wa Simiyu ambayo ilikuwa
imalizike kesho kutokana na msiba wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Maswa ambayo alipangiwa kuitembelea leo.
Mkurugenzi huyo Bw. Traceas Kagenzi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana kutokana na shinikizo la damu. Atasafirishwa kwenda Muleba kwa mazishi.
Mkurugenzi huyo Bw. Traceas Kagenzi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana kutokana na shinikizo la damu. Atasafirishwa kwenda Muleba kwa mazishi.
Akitoa salamu za rambirambi
kwenye ibada ya kumuombea marehemu Kagenzi iliyofanyika nyumbani kwake
Maswa mjini, Waziri Mkuu alisema ameshtushwa na msiba huo uliotokea
ghafla na kwamba Taifa limempoteza mtumishi mahiri ambaye bado Taifa
lilikuwa likimtegemea.
“Nimeshtushwa sana na taarifa za msiba huu. Nimeambiwa hadi juzi usiku alikuwa akishirikiana na Mkuu wa Wilaya hii kuandika taarifa ya ziara ya wilaya hii. Kwa niaba ya Serikali, ninawapa pole sana wafiwa na Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi,” alisema.
“Nimelazimika kukatisha ziara ya mkoa huu kwa sababu huyu ni mtumishi mwenzetu.

Tags
HABARI KITAIFA