Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) na Makamu wa Rais wa
Shirika la Koica la nchini Korea Kusini, Taemyon Kwon, wakiweka tofali
kwa pamoja kuashiria uweka wa jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika
iliyopo Manispaa ya Ilala, inayojengwa kwa ufadhili wa nchi hiyo Dar es
Salaam jana. Ujenzi huo hadi kukamilika utagharimu sh. bilioni 8.8 za
kitanzania.
Hutuba na taarifa ya mradi huo zilisomwa.
Balozi wa Korea nchini Geum-young Song (katikati), akizungumza katika hafla hiyo.
Wananchi wa Chanika wakiwa kwenye hafla hiyo ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali yao.
Diwani
wa Kata ya Chanika, Mr Massaburi akitoa neno la Shukurani kwa RC
Makonda, Serikali pamoja na Serikali ya Korea kwa ujenzi wa Hospitali
hiyo.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala, Mr Isaya (kulia), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Grace Magembe, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Victriana
Ludovic na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo Mr Kim wakiweka
jiwe la msingi la Hospitali hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanika wakiwa kwenye hafla hiyo.
Meneja
wa Mradi huo, Mr Kim akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda na ujembe wake ramani ya majengo ya Hospitali hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanika wakitoa burudani katika hafla hiyo.
Wasanii wakitoa burudani katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Manispaa ya Ilala na Korea Kusini
……………………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
……………………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na balozi wa Korea nchini
Geum-young Song wameweka jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika Manispaa
ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapaaaaaaaaaao itakapo kamilika itakuwa
na uwezo wa kuhudumia wananchi 4000.
Akizungumza
katika hafla ya kuweka jiwe hilo la msingi Chanika jijini Dar es Salaam
jana, Makonda aliishukuru serikali ya Korea kwa msaada wa ujenzi wa
Hospitali hiyo ambayo itawasaidia wananchi wa Chanika na kupunguza
msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Amana.
“Tunawashukuru
hawa ndugu zetu wa Korea Kusini kwa msaada wa kutujengea Hospitali hii
nawaombeni wananchi kuitunza ili kila mtakapokuwa mnafika kutibiwa
tuwakumbuke wakorea” alisema Makonda.
Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Victorina Ludovic alisema ujenzi wa
Hospitali hiyo utasaidia kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi
wapatao 398,882 kutoka maeneo ya Chanika, Msongola, Zingiziwa na Majohe
hivyo kupunguza muda na gharama ambazo wananchi wamekuwa wakitumia
kufuata huduma hizo umbali wa kilometa 30 kwenda hospitali ya Amana ya
Rufaa.
Ludovic alisema ujenzi wa mradi huo hadi utakapokamilika utagharimu dola la milioni 4 sawa na sh.bilioni 8.8 za kitanzania.
Balozi
wa Korea nchini , Geum-young Song amesema wakorea hawafurahishwi
wanapoona mama na mtoto wanapoteza maisha wakati wa kujifungua nchini
Tanzania.
“Nchi
yetu kupitia shirika la Koica imeamua kujitolea kujenga hospitali hii
ili kuwasaidia wananchi wa Tanzania kupata huduma bora ya afya ya mama
na mtoto wakati wa kujifungua kwani hatupendi kuona wanapoteza maisha
wakati wa kujifungua” alisema Young Song.
Balozi
huyo aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na nchi ya Korea
katika shughuli mbalimbali jambo linaloimarisha uhusiano baina ya
wananchi wa nchi hizo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Tags
HABARI KITAIFA