Huyu jamaa ni maarufu sana kwa kuwadhihaki wachezaji wa
Real Madrid pale ambapo watakapo fanya vibaya kwenye kitu chochote hasa
cha kuhusu soka.
Gazeti la Marca limetoa taarifa kwamba Pique ni moja kati
ya watu ambao wanai motivate wachezaji wa Real Madrid kutaka kuifunga
Barcelona. Pique amekua bingwa wa kuchokoza Real Madrid kwenye internet
mara baada ya kupoteza mechi.
Pique aliwahi kuwachokoza Real Madrid walipotolewa kwenye
michuano ya Copa del Rel. Pia aliwahi kuzomewa na mashabiki wa Real
Madrid alivyokua kwenye majukumu ya timu ya taifa.
Wachezaji ambao ana beef nao sana ni pamoja na Ronaldo,
Sergio Ramos na Arbeloa na hawa inasemakana wamepanga sana kuhakikisha
wanaifunga Barcelona.
Lakini swali juu ya hii ripoti ni kwamba Gerard Pique ndio
itakua chachu pekee ya Real Madrid kushinda? Mechi itakua Live kwenye
Azam TV saa 3:30 leo usiku.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA